TOFAUTI YA CHAMA CHADEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA) NA CHAMA CHA MAPINDUZI (C.C.M)
UTANGULIZI
Wazo la kuandika katiba mpya lilikuwa ni wazo la CHADEMA kupitia mgombea wake Dr. Willibroad Peter Slaa. Wala halikuwa wazo la C.C.M wala mgombea wake Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
1. Tofauti ya “kwanza” ipo kwenye jina la vyama hivyo,wakati CHADEMA ni chama cha Demokrasia namaendeleo. Wao C.C.M ni chama cha kupindua mambo yote mazuri a.k.a kuyakataa na kuunga mkonomambo mabaya (ufisadi).
2. Wakati CHADEMA tunaunganisha nguvu za viongozi wetu kupiga vita “UFISADI”.
Wao C.C.M wanaungisha nguvu za viongozi wao kuwalinda “MAFISADI”.
3.Wakati CHADEMA tunalinda rasilimali za umma (madini, misitu na wanyama) zisichukuliwe na wanaojiita wawekezaji. Wao C.C.M wanawalinda wawekezaji (wachukuaji) iliwaendelee kuchukua rasilimali za umma.
4.Wakati wabumge wa CHADEMA walipopinga tozo ya line za simu ambazo zitaumiza wananchi. Wao C.C.M waliunga mkono tozo hizo za line za simu kwa mbwembwe.
5.Wakati CHADEMA tunataka haki za binadamu na maadili ya viongozi viingie kwenye katiba mpya inayoandikwa na wananchi. Wao C.C.M wanapinga haki hizo zisiingie kwenye katiba.
6.Wakati CHADEMA tunataka tume huru ya ukaguzi.Wao C.C.M wanasema tume hii tuliyonayo inafaa.
7.Wakati CHADEMA tunaunga mkono Rasimu ya katiba,yenye maoni ya wananchi yene muundo wa Serikali tatu. Wao C.C.M wanaipinga Rasimu hiyo yenye maoni yawananchi.
“Rais Kikwete ndiye aliyeanzisha mchakato na yeye ndiye aliyesaini Rasimu ya pili mwanzo wa Rasimu na mwisho wa Rasimu.
Na Kikwete huyo huyo ndiye aliyekuwawa kwanza kukataa jambo alilolikubali kwa kusainimwenyewe”.
Na Mwl Anthony Thomas Gella – 0764
632731/0656907751
Email: agella72@yahoo.com
No comments:
Post a Comment