-Ndani ya kipindi kisichozidi miezi 6 Kumeripotiwa wizi wa zaidi ya Bilioni 650 ndani ya Hazina na B0T,kunaripotiwa huku viongozi waandamizi wa serikali na chama cha mapinduzi wakihusishwa moja kwa moja,
-Daima Taifa limeelemewa na mfumo wa kifisadi ambao kwa namna moja ama nyingine umechangia Ukuaji wa Deni la Taifa amblo limefikia Trilioni 40.6,Deni hilo ni sawa na kusema kila mtanzania anadaiwa shilingi 470,000.
-Mpaka leo hamna maelezo yakutosha kuhusiana na waliokwapua Bilioni 450 hazina na Sasa kuchotwa Bilioni 200 B0T ambzo zinadaiwa kutumika katika chaguzi za Kalenga na Chalinze pamoja na kuwahonga wajumbe wa Bunge la katiba zikitumiwa na CCM ili kuwashawishi wajumbe kupindua msingi wa rasimu ambao ni serikali tatu.
-Ni dhahiri tumefanywa mazuzu na watawala na wale ambao kwa namna moja ama nyingine wananufaika na mfumo wa kifisadi pamoja na jamaa zao na ndio maana hta ndani ya rasimu wanapinga uwajibikaji kuwa sehemu ya tunu za taifa na sio kwa bahati mbya ni mkakati wa kulinda mfumo.
-Watanzania ifike mahali bila kujali itkadi tupase sauti kuu na vitendo kwa watawala la sivyo tutajikuta tumeelemewa na mizigo ambyo imenufaisha wachache na jamaa zao,Tunahitaji mabadiliko makubwa ya kifkra,kimfumo na kisiasa kwa kuwa hatuna chaguo lingine pasi na kung'oa utawala uliokosa uhalali wa kulinda rasilimali za umma.
No comments:
Post a Comment