Na Liberatus Mwang'ombe "Libe"
Suala la muungano limejaa mauzauza mengi kiasi kwamba watawala
wanashindwa kujibu maswali na hoja za msingi juu ya muungano huu.
Wanacho
kifanya ni kuwatishia wananchi kuwa jeshi litachukua nchi au Sultan atarudi
Zanzibar. Huu ni uongo na upotoshaji mkubwa. Hili swala muungano wa nchi zetu
mbili lina leta maswali mengi kuliko majawabu.
Nitafanya
uchambuzi kidogo wa muungano wetu huu batili. Kwa kifupi nchi inayo itwa
Tanzania ni batili. Ubatili wake unakuja pale ambapo ilianzishwa na mtu moja,
Nyerere, bila kushirikisha upande wa pili ( Zanzibar na Bunge laki): hata
waTanganyika hawakushirikishwa.
Ili
muungano uwe harali kisheria, ni budi hati ya muungano iwe ratified na Bunge la
Zanzibar. Ukweli ni kuwa Bunge la Zanzibar halijawahi kupitisha hiyo hati. Hadi leo
hiyo hati haipo kwenye hansard ya Bunge la Zanzibar, Nyerere alitumia ubabe
kuwalazimisha Zanzibar muungano; kwa kweli sijui malengo yake yalikuwa ni
nini!!! Ubabe
huu unadhihirika pale alipo lazimika kuiuwa Tanganyika na kutunga
"decree" tatu baada ya yeye kukutana na Karume. Tunajua decree
hutungwa na nchi iliyo chukuliwa na jeshi. Nyerere
kwa ubabe wake alibadilisha mambo ya Tanganyika kuwa ya muungano, mfano, nembo
ya Tanganyika ikageuzwa ya muungano, office za Tanganyika zikageuzwa za
muungano, Katiba ya Tanganyika ikawa ya muungano, mahakama kuu kuwa ya muungano
nk.
Haya yote
alifanya yeye binafsi kwa amri (decree) bila kuwashirikisha waZanzibar (Bunge
la Zanzibar) wala waTanganyika. Huu ni udicteta. Kwa
history hii kama kuna mtu atakuwa anashangaa kwa nini waZanzibar wana chuki na
Nyerere na Tanganyika; atakuwa close minded na hataki kuukabili ukweli. Zanzibar
ni nchi ambayo ilikuwa huru kabla ya muungano na sasa imesema haitaki huu
muungano wa mauzauza. Utailazimisha muundelee kuungana nayo? Tuwe wakweli,
wapenda haki na wahalisia.
The only
way tutaweza kuishi kwa amani na Ndg zetu waZanzibar ni kuipa Zanzibar mamlaka
kamili au kudisolve huu muungano batili. Serikali mbili au moja WONT WORK. Tatu ndio
jawabu. Otherwise; muungano huu batili ni time bomb ambalo lina subiri kulipuka
muda wowote
Kumbukeni;
Zanzibar ni nchi kamili kama Kenya na Uganda; ilipata Uhuru wake kwa kumwaga
damu, sio kama sisi tulipata kwa bwerere na ndio maana akili zetu hazitaki
kukabili ukweli. Zanzibar
ina Rais wake na Kikwete leo hii akienda Zanzibar hana sauti; huenda kam
mualikwa (mgeni). Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano Mizengwe Pinda huwa
hakanyagi Zanzibar ( kuna mtu amewahi sikia Pinda kaenda Zanzibar kusimamia
miradi ya maendeleo?). Hii inazihirisha pasi na shaka kuwa Pinda sio Waziri wa
muungano, bali wa Tanganyika.
Tanganyika
ipo ila watawala dharimu wa CCM wanaiogopa. Leo hii
Kikwete akienda Zanzibar hapigiwi mizinga 21; Dr. Shein ndio anapigiwa. Sasa
hapo Mkuu wa nchi ni nani? Shein au Kikwete? Lazima
kama vijana wa kizazi kipya, tujifunze kudadisi na kusaka ukweli; sio kubuluzwa
na haya MA CCM ambayo yameishiwa mbinu za kutawala na kubaki kutumia mabavu
TAFAKARI.....
No comments:
Post a Comment