Katibu
mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Dk. Willbroad Slaa ambae pia
ni kiongozi wa msafa a UKAWA kanda ya kaskazini amesema licha ya kuwepo kwa
mvutano wa muundo wa serikali kwenye katiba mpya, katiba ya mwaka 1977
inayotumika sasa ina mfumo wa serikali tatu.
Dk. Slaa amesema hayo wilayani Bunda
mkoa wa Mara kwenye mkutano wa Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA ambapo amesema
katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 inayotumika hivi sasa inabainisha wazi mambo
ya muungano na yasiyokuwa ya muungano na kwamba katiba hiyo imeweka wazi mfumo
wa serikali ya Zanzibar hivyo wajumbe wanapaswa kupitisha rasimu ya katiba mpya
ili kuiweka Tanganyika hadharani kama ilivyo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment