Mkutano wa
CHADEMA ulio fanyika leo Mei 28, 2014, wilayani Mbarali ukiwa na agenda zifuatazo uliingia dosari pale Mbunge wa
Mbarali Mh. Kirufi alipo itisha mkutano eneo hilo hilo ambalo CHADEMA ilibidi
wafanye mkutano wao. Ikumbukwe kuwa CHADEMA ilitakiwa kufanye mkutano Mei 25,
2014, lakini polis walizui kwa madai kuwa intelejensia sio nzuri na wakasogeza
mkutano siku ya leo Mei 28,2014
Agenda za
mkutano zilikuwa kama zifuatazo
-Ushuru
ulio pitishwa na madiwani wa CCM wa gunia la mpunga
-Katiba na
UKAWA
-Taarifa ya CAG juu ya ubadhirifu wa Billion mbili na million
mia nne (2 billion na million 400) fedha za halimashauri
Mkutano huu ulio kuwa ukiongozwa na mwenkiti wa CHADEMA wilaya,
Ndg. Peter Mwashiti, na kuhudhuriwa na Madiwani wote wa CHADEMA wilayani
Mbarali uliingia dosari na kuchelewa kuanza pale ambapo Mbunge wa Mbarali Mh.
Kirufi alivyo itisha mkutano eneo moja karibu na mkutano wa CHADEMA.
Uongozi wa CHADEMA wilayani Mbarali ulipo ona Mbunge huyo
kaitisha mkutano; ulienda polis na kuonana na OCD kuomba kibali cha uhalali wa
Mbunge Kirufi kufanya mkutano siku moja na eneo moja la mkutano wa CHADEMA. OCD
aliomba apewe muda na uongozi wa CHADEMA ili aongee na RPC. Baada ya maongezi
ya muda mrefu na RPC, OCD alikili kuwa Mbunge kirufi alikuwa afanye mkutano
wake siku nne zilizopita, Mei 24, 2014 na hana uhalali wa kufanya mkutano siku
ya leo.
Baada ya majadiliano hayo, OCD alitoa amri kuwa Mbunge Kirufi
asitishe mkutano wake. Mh. Kirufi alitii amri hii na CHADEMA iliendelea na
mkutano wake kama kawaida. Mkutano wa CHADEMA ulimalizika kwa amani na
wanaMbarali wakiwa wamepata muongozo juu ya UKAWA, ushuru wa gunia na
ubadhirifu wa billion mbili na million 400.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Wilayani mbarali Ndg Peter Mwashiti
anatoa shukrani za dhati kwa wote walio hudhuria mkutano huo.
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbarali, Peter Mwashiti
Habari na Nickodemas kutoka Mbarali
No comments:
Post a Comment