Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, April 3, 2014

Wajumbe Bunge maalum;“Akili za kuambiwa changanya na zako.”

Na Bryceon Mathias

WAPO Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walioambiwa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wasigombee Ubunge kwa Tiketi ya Chadema ila CCM, lakini walipochangana na Akili zao sasa ni Wabunge Chadema.

Lakini pia wapo Waliotumia Akili za kuambiwa wakagombea Uongozi wa Tiketi CCM, walitolewa kwenye Kura za Maoni na sasa hawana Ubunge bali wamebaki kuwa kama Karai la Zege ambalo kazi yake ni kujenga nyumba lakini mwisho linatupwa nje kama takataka.

Aidha miongoni mwa Viongozi fulani fulani huko nyuma, baadhi ya watu walidhani kwamba hawana uwezo wa kuongoza umma kwa sababu zao binafsi kiasi cha kuogopa kugombea uongozi; Llakini walipothubutu akili za kuambiwa wakachanganya na za kwao, leo ni Viongozi.

Hivyo hata kama CCM Kinawalazimisha watu kwa nguvu kuwaambia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba waunge mkono Serikali Mbili na Kura ya Uwazi, badala ya Rasimu ya Serikali Tatu  na Kura ya Siri, na wao wachanganye na akili zao.

Simba mmoja anayeongoza Kundi la Kondoo 100 katika Vita, ana Ushini Mkubwa kuliko Kuni la Simba 100 wanaoongoza Kondoo mmoja! Samba hao ni pamoja na wale wana CCM ambao pamoja na kulazimihwa kuweka wazi upigaji kura wao, wanaidai Tanganyika hadharani.

Ingawa wako Kondoo 100 wa Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini (UWAKA) dhidi ya CCM wanaoongozwa na Simba Mmoja yaani Tanganyika katika Msuguano wa Marekebisho ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya, wako wengine ndani ya Chama Tawala wanaofanana nao.

Mfano wa Simba Mmoja huyo anayeongoza Kundi la Kondoo hao 100 dhidi ya Kundi la Simba 100 likiongoza Kondoo mmoja ni pamoja na Mbunge waKahama na aliyekuwa Mwenyekiti Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli (CCM).

Kimsingi huwa tunamshangaa mtoto akisha kuwa limbukeni akiwa mjini; anapoanza kuwakataa wazazi wake kwamba sio waliomza, eti kwa sababu tu amekutana na waliommshauri kumwambia fanya hivi na fanya kile bila kuchanganya na akili yake.

Ni wakati muafaka sasa watanganyika tusimkatae Baba na Mama yetu Tanganyika aliyetuzaa na kutukuza, eti kwa sababu ni Wazee!
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeamua kufia kwenye hoja yake ya muundo wa Muungano wa serikali mbili.

Vikao vya juu vya chama hicho - Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Kamati kuu (CC) - vilivyofanyika mwezi uliopita mjini Dodoma, vimesisitiza umuhimu wa kuendelea na Muungano wa serikali mbili kwa madai kuwa hiyo ndiyo sera ya chama hicho.

Hata andishi la CCM, lililowasilishwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba, limepinga mapendekezo ya kuwapo kwa serikali tatu ndani ya Jamhuri ya Muungano
Andishi linasema, mwarobaini wa matatizo ya Muungano, siyo kuwapo kwa serikali tatu bali serikali mbili.

Katika kutetea mfumo wa serikali mbili, chama hicho kimejikita kwenye hoja tatu:

Kwanza,muundo wa Muungano wa serikali tatu ni kinyume cha makubaliano yaliyofikiwa Aprili 1964 na waasisi wa Muungano, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume.

Pili, Muungano wa serikali tatu utaongeza gharama serikalini; utaingiza nchi kwenye umaskini na utasababisha Zanzibar kushindwa kuchangia uendeshaji wa serikali ya pamoja. Hoja inayojengwa ni kwamba mapato ya Zanzibar ni madogo ukilinganisha na Tanganyika.

Tatu, mfumo wa Muungano wa serikali tatu, siyo sera ya chama hicho tawala. Kinasema sera ya CCM ni serikali mbili kuelekea serikali moja. Inadai kuwa mfumo wa serikali tatu unahatarisha uhai wa Muungano.

Ukichunguza hoja hizi za kupinga Muungano wa serikali tatu na utetezi wa serikali mbili,waweza kuona jinsi chama hiki kinavyozeeka kwa kasi; kinashindwa kufikiri,kuchambua na kutafiti.

No comments: