“Mkuki kwa Nguruwe, kwa Binadamu Uchungu”
Na Bryceson Mathias
HIVI karibuni Chama cha Mapinduzi (CCM) kilitoa walaka unaojadili Mapendekezo ya Katiba mpya nje ya Bunge Maalum la Katiba na kuujadili kwenye vikao vya Umoja wa Wabunge wa CCM (Part Cocas); Je huo si Uhaini au Uasi kama anaodai Dk. Chrisabt Mzindakaya kwa UKAWA?
Wakati hayo yakifanyika Mwanasiasa Maarufu nchini Dk. Mzindakaya, hakuthubutu kujitokeza kuwahoji wabunge wa Chama chake (CCM) kuzungumzia na kuijadili Katiba hiyo kwenye ‘Part Cocas’ nje ya Bunge Maalum, ilihali vikao vya Katiba hiyo tayari vilikuwa vimeanza bungeni.
Mwana siasa huyo huyo {Dk. Mzindakaya), mapema wiki iliyopita akizungumza na Waandishi wa habari, alikurupuka na kuutupia Makombara Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa kuzungumzia Mjadala wa Katiba nje ya Bunge Maalum.
Dk. Mzinakaya alisema, “Uamuzi wa UKAWA kuzungumzia kuendeleza mazungumzo hayo nje ya Bunge ni Uhaini wa Kisiasa na hawana uhalali wa kudai kuwa wanawawakilisha watanzania wote”.alidai.
Mzindakaya alihoji takwimu zilizotolewa na Tume ya Marekebisho ya Katiba zilizodai watu wengi walipendelea muundo wa Serikali Tatu, huku akiacha kumhoji Mwenyekiti wake wa CCM Jakaya Kikwete kwa nini aliiteua Tume hiyo na kuridhia kila walichomshirikisha katika kazi yao.
Hata hivyo Mzindakaya alijaribu kuunanga UKAWA akiushutumu kwa kutaka kuzungunguka nchi nzima ili kuhakikisha unawaelimisha wananchi mambo wanayopaswa kuelewa kuhus mchakato unaoendelea, ili utakapofika wakati wa kukataa au kukubali Katiba iliyopendkezwa, wawe na Uelewa Mpana na Elimu ya kutosha.
Alichofanya Mzindakaya kwa kuzungumza na Wandishi wa Habari, hakina toauti na cha ‘Part Cocas ya CCM, UKAWA na hata kile cha baadhi ya Mawaziri waliotuhumiwa kuwafanyia Karamu ya Vinywaji na Vyakula kwa baadhi ya wajumbe wa Asasi na Taasisi za Katiba hiyo.
Nasema hivyo kwa sababu hata Mzinakaya mwenyewe amefanya makosa kwa sababu amezungumzia suala la Katiba hiyo nje ya Bunge hilo hivyo nay eye mwenyewe anaanya Uhaini wa kisiasa maana hana kibali cha Mwenyekiti wa Bunge hilo au ridha ya Wajumbe wake.
Sisemi baadhi ya Wajumbe wenye maslahi binafsi kama Mzindakaya waache Unafiki la hasha, bali nasema wawe waadilifu wa kweli kwa sababu tunataka kujifunza kwao. Kama watakuwa ndumila kuwili wakitangaza Sera kijamaa halafu wanatekeleza Kibepari ni Aibu kwa Taia hili.
Ni aibu kwa Taifa kwa sababu, waswahili wanasema alivyo Mfalme, Mtawala au Baba na Mama; Ndivyo walivyo wafuasi wao. Kizazi hiki kama hakuna uangalifu wa kutosha, kitarithi Ufisadi, Rushwa zilizokithiri, Unyama wa kutisha na Ujangili wa Kisiasa maisha yetu yote.
Tutapata aibu kutokana na kudhani kwamba, wapo waliotutangulia wanaoweza kutusaidia na kuwa msaada kwa kizazi kinachokuja ili kiige, kumbe tunaambulia kuiga patupu.
Mzindakaya katika hoja zake alidiriki kudai, UKAWA kwenda kutoa Elimu kwa wananchi, watakuwa wanatumia muda na rasilimali ya nchi vibaya; Je Part Cocas na Karamu zinazodaiwa kufanywa na Mawazir kwa Wajumbe wa Katiba, hazitumii vibaya rasilimali hizo kama UKAWA? .
Ni Rai yangu kwa Mzindkaya aelewe kwamba, Viongozi wetu walio wengi nchini wanaandaa Sera Kijamaa, lakini wakati wa utekelezaji wanatekeleza Kikoloni na kuwatetea au kuwabeba waovu. Tuache mtindo huo Sugu, Mkongwe na wa aibu usiohofiwa wala kwisha. .
No comments:
Post a Comment