Wote wawili ni
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.Wote wawili ni Wabunge vijana kabisa tena
wenye uelewa mkubwa. Wote wawili ni Wabunge machachari katika kujenga hoja na
kutetea mnachokiamini.Wote wawili ni kati ya Wabunge watumiaji wakubwa wa
mitandao na vyombo vingine vya habari. Nyinyi ni mfano wetu sisi vijana katika
kuonyesha ya kuwa sisi vijana tunaweza.
Leo, mmechomoza
'twitter' na kuandika maoni yenu juu ya Hotuba ya Jaji Joseph Sinde Warioba
alipowasilisha Rasimu ya Katiba Bungeni. Naamini wote mlikuwepo Bungeni na
kupata nafasi nzuri na ya mwanzo katika kusikiliza na kuelewa alichokisema Jaji
Warioba. Nyinyi mlipaswa kuelewa zaidi na kuja kutuelekeza na sisi. Lakini,mna
nia ya kupotosha ukweli.
Wote mnajenga
hoja kuwa Jaji Warioba ana nia ya kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mmeitumia Hotuba ya Jaji Warioba kujengea hoja zenu. Ndugu Makamba umekwenda
mbali zaidi na kusema kuwa CCM itatumia wingi wake kuulinda Muungano. Unajaribu
kuuaminisha umma kuwa Jaji Warioba anatoa hoja ya kuuvunja Muungano uliopo.
Mahali gani
aliposema nia ya kuuvunja muungano? Mahali gani aliposema hautaki kuuona wala
kuusikia muungano uliopo? Hapa mnajaribu kupotosha.Na hamtaweza. Kwasasa tuna
uelewa na ufuatiliaji wa kutosha. Si rahisi kuturubuni na kutupotosha.
Baniani
mbaya,kiatu chake dawa!
Msewela E. Petro/JF
1 comment:
Na ndio hao hao wana vaa suit za $120 na kujidai wakombozi wa watanzania. Wanaishi maisha ya kukufuru nchi Tanzania haklafu wanajidai wao ni wakombozi wa wananachi.
Makamba na Zitto ni watu wakuangaliwa sana wanajidai wana upeo mkubwa lakini hawawa zazidi ya kudanganya wajinga Tanzania.
Ujana wao usiwe kigezo cha kulinda wanayoyajua yao.
Post a Comment