Na Bryceson Mathias
KATIKA hali inayoonesha kuwa wananchi nchini wanakatishwa tamaa na mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba kuhusu kukamilika kwa Mjadala wa Marekebisho Rasimu ya Katiba Mpya, Wengi wameshauri Rais Jakaya Kikwete, alifute na kuliondoa Bunge hilo ili lisiangamize Taifa na kulifanya kama Chuo cha Matusi.
Wengi wa waliotoa maoni kwa mwandishi wa Makala hii hasa kutoka katika Taasisi za Dinii, Vyuo, Wafanya Biashara, Wakulima, Wafugaji, Wanasheria kwa wananwake na wanaume, wanadai Utoto unaooneshwa na Wajumbe hao wakiwa bungeni, una nia ya kuliangamiza Taifa.
Wamedai ingawa kusudi la Rais inawezekana lilikuwa Jema likiwa na nia ya Kulijenga Taifa na kuliingiza katika Historian na Ramani ya Ulimwengu, lakini uelewa mdogo wa baadhi ya Wajumbe hao, hauna nia njema hasa kwa mustakabali, Uchumi na Maendeleo ya nchi.
Mchungaji wa Kanisa la Uponyaji la Lusanga Mji Mdogo wa Madizini Mtibwa, Salvatory Vicenti, alisema, Utoto unaofanya na baadhi ya Wajumbe hao wakiwa bungeni humo, hauma tofauti Mgonjwa anayekataa Chakula hali akijua atakufa, hivyo amemtaka Kikwete kuwafuta na kuwaondoa Wajumbe hao nchi isiangamie kiuchumi.
Akikazia kauli yake kwa Neno la Mungu, Mchungaji Visenti alinukuu Maandiko ya Biblia Kitabu cha kwanza cha Timotheo 5:8 kinachosema, “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini”.
Alifafanua akisema kama Baba au Mama anaweza kuamua kwa makusudi kula Chakula na kujiwekea Kingi huku akiwapa kidogo watoto wake au kuwanyima kabisa, Baba au Mama huyo hafai kulea Familia; na hivyo ndivyo ilivyo kwa wajumbe hao kudai posho kubwa hawatufai kwa Taifa.
Alisema, Wakati Kanisa na Taasisi zingine za Dini zikiomba Amani katika kazi hiyo Maalum waliyoteuliwa na Rais kuna baadhi ya Wajumbe wanayofanya bungeni humo ni kama wanafanya kusudi ili zitokee Vurugu kwa maslahi yao binafsi.
Alionya kwamba, isije ikawa kwa kuwa kuwepo kwa Katiba Mpya haikuwa Ajenda ya Chama cha Mapinduzi (CCM), na Rais Kikwete ameiridhia ili kuendana na wakati, isije ikawa wamo watu miongoni mwa Chama chake, wanaamua kufanya hivyo kwa makusudi maana tunaowaona wakiwa na vituko na utoto ni wateule wake.
Mchungaji Vicenti aliwanyoshea Kidole wajumbe hao akidai kwamba,, kama watathubutu kujidanganya kutummia Mchakato huo wa Katiba wakidhani wanawaangamiza watanzania, waelewe kuwa wataangamia na wao maana Katiba hiyo itatumika kwetu, kwao na watoto wao.
Hata hivyo alishauri kwamba, kinachowasumbua wajumbe hao ni pamoja na uroho na tama ya vyeo katika uchaguzi wa mwaka 2015, ambapo alisema, kutokana na kuwa na makundi ya Urais, Ubunge na Udiwani kwa uchaguzi huo, umepelekea hata murua wa Mjadala wa Rasimu kuharibika.
Mchungaji huyo aliwaponda wajumbe hao akisema, anashangazwa kuona pamoja na Heshima kubwa waliyopewa na Rais Kikwete, kuwateua miongoni mwa watanzania Milioni 45 ili kuoresho ya Katiba hiyo, wamejisahau na kuona wao ni muhimu kuliko wananchi na Rais.
Aliongeza kwamba, tatizo linguine linalobishaniwa ni Muungano jambo ambalo ameshauri ni heri tangu ingepigwa kwanza kura ya maoni ya wananchi, wanataka Serikali ya aina gani, Moja, Mbili au Tatu ndipo yafanyike maboreho mengine kuliko kuharibu uchumi na Kodi ya wananchi, ambapo Vicenti alikemea Tamaa na Uroho wa Madaraka kuwa ni sawa na Mtu Mvivu ambapo alinukuu maandiko ya Mithali 6:6-9
No comments:
Post a Comment