DIASPORA IN USA TELECONFERENCE MARCH 20, 2014, 8PM
Waheshimiwa Wanadiaspora,
Viongozi wa Jumuiya za Watanzania za Marekani wakishirikiana, ZADIA na DICOTA,
wanapenda kuwatangazia kuwa kutakuwa na teleconference siku ya Alhamisi tarehe
20 Machi kuanzia saa mbili usiku(8:00PM) kwa saa za Eastern Time.
Lengo ni kuwapa muhtasari wa masuala yanayoendelea kule Dodoma kwenye Bunge
Maalum la Katiba na kuwafahamisha mpaka sasa tumefikia wapi katika
kuhakikisha suala la uraia pacha linaingizwa kwenye katiba mpya ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Watanzania na Watu wenye asili ya Kitanzania wanaoishi Marekani wote mnaombwa
kuudhuria.
Ili uweze kushiriki kwenye Teleconference hii piga namba 712-432-1500 halafu
ingiza pin namba ikifuatiwa na alama ya reli kama ifuatavyo: 465228#.
Wote mnakaribishwa!
Diaspora Constitution Petition- FUNDING: click here kuchangia...
Imetolewa na:
Viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Marekani, ZADIA na DICOTA.
Tarehe 18 Machi 2014
No comments:
Post a Comment