Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, February 26, 2014

Mnyika ataka uwazi ufuatiliaji posho


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, John Mnyika (pichani), amemtaka Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Ameir Pandu Kificho, kuwasilisha taarifa ya kazi zilizofanywa na kamati ya kufuatilia posho na kanuni ili iwe wazi kwa wajumbe na jamii. Kadhalika, alisema usiri, udhaifu na uzushi uondolewe mjadala ni Katiba mpya na siyo posho.

Katika taarifa yake, alisema usiri na udhaifu wa uongozi wa Bunge katika kutoa taarifa na uzushi wa baadhi ya viongozi au watendaji wa serikali na baadhi ya wajumbe umesababisha majalada wa Rasimu ya Katiba kubadilika na kuwa posho.

Alisema ili kulirudisha Bunge Maalum katika mkondo sahihi kwa kujadili kanuni na rasimu ni vyema Katibu wa Bunge na Baraza la Wawakilishi watoe taarifa ya ziada ya kazi ambazo kamati za muda za uongozi na kanuni za kumshauri zimefanya.

“Makatibu wasipofanya hivyo, Mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho, atumie ufunguzi wa semina ya kanuni za Bunge kueleza kazi kubwa iliyofanywa na namna ambavyo kwa ukubwa wa kazi muda umeongezwa na muda wa ziada wa kuwasilisha kanuni zilizofanyiwa marekebisho,” alisema.

Kitomory S./ Ippmedia-Nipashe

No comments: