Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, February 21, 2014

Membe aichoka CCM

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amekikejeli Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba kinaufanya uchaguzi wa rais kama uchaguzi wa kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani (Papa). Membe alitolea mfano wa uchaguzi wa Papa jana wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kupata maoni na hatima yake kisiasa, baada ya CCM kumfungia kwa miezi 12 na kumuweka chini ya uangalizi, baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kukiuka kanuni za chama hicho kwa kuanza mbio za urais mwaka 2015 mapema.

Waziri Membe alisema kuwa mataifa mengi duniani yameiga mambo mengi yakiwemo mavazi ya majaji, wanasheria na spika wa bunge kutoka utamaduni wa Kirumi unaotumiwa na kanisa hilo, lakini yameshindwa kuiga uchaguzi wa Papa.
Tanzania Daima

No comments: