Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, February 6, 2014

MABOMU YALINDIMA MOROGORO; WAFUGAJI VS WAFUGAJI


MABOMU ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji



Wakulima hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali sehemu za siri na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha msongamano mkubwa wa magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa.
Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaaamuru vijana wake wawatawanye wakulima hao ambao waligoma na kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea polisi kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.
Wananchi takribani 20 wamekamatwa na polisi katika vurugu hizo.
Kwa sasa hali kidogo imetulia na magari yameanza kupita eneo hilo.Chanzo DJ Sek Blog

No comments: