Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, February 25, 2014

CHADEMA yataka posho za wajumbe zikatwe kodi


    Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshangazwa na uamuzi wa serikali wa kuwalipa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba posho ya Sh. milioni tisa kwa mwezi, huku ikiacha kuwatoza Kodi ya Mapato (Paye) kutoka katika fedha hizo, kinyume cha sheria za nchi.

 Pia kimewashangaa wajumbe hao, ambao ni watunga sheria mama ya nchi (katiba) kuwa wavunjifu wa sheria ya kodi kwa kutolipa kodi.

 Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa Chama hicho, John Mrema, alisema: 

“Haiwezekani (wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba) walipwe milioni tisa kwa mwezi bila kukatwa kodi wakati mwalimu analipwa 298,000 kwa mwezi na anakatwa kodi.”



      Alisema daima katiba ya nchi hutakiwa kutungwa na wazalendo na kwamba, kipimo kimojawapo cha uzalendo ni pamoja na kulipa kodi ili kutekeleza sheria za nchi bila shuruti na kuwataka wajumbe wote wa Bunge hilo kulipa kodi hiyo kwa mujibu wa sheria. 

 Pia aliitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya kodi ya mapato kwa mujibu wa sheria za nchi. 

“Haiwezekani watunga sheria mama wawe wavunjifu wa sheria ya kodi. Hiyo katiba wanamtungia nani akaitekeleze kama wao wenyewe siyo watiifu wa sheria za nchi?” alihoji Mrema.

Aliongeza: “Ni wakati sasa wa TRA kuonyesha kwa vitendo na siyo kuwaumiza wafanyabiashara wadogo na wafanyakazi kwa mashine zao za EFD, huku wanasiasa wakiachwa bila kodi.”

Muhibu S. /Ippmedia-Nipashe

No comments: