Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, February 14, 2014

CHADEMA yamteua Mwenda ubunge Kalenga

 CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemteua mwanasheria Sinkala Mwenda kugombea ubunge wa Kalenga baada ya kuwashinda wenzake 13. Katika kinyang’anyiro cha uteuzi huo kada aliyekimbia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kushindwa kura za maoni mwaka 2010, Zubery Mwachura, aliambulia kura sifuri. Mwenda alitangazwa kuwa mshindi  baada ya uchaguzi uliofanyika juzi kwa zaidi ya saa 10 mjini Iringa. Uchaguzi huo ulisimamiwa na wajumbe  wa Kamati Kuu ya CHADEMA taifa, Chiku  Abwao  na Benison Kigaila, ambapo kura 132 zilipitisha jina la mwanasheria huyo huku kura 122 zikimchagua Grace Tendega.

        Katika uchaguzi huo, kada wa CHADEMA na muuza magazeti maarufu mjini  Iringa, Aidan Pungili, aliambulia kura 2 wakati Daniel Luvanga akipata kura moja. Wagombea wengine walioonyesha  kufanya vema baada ya  kujiunga na CHADEMA  wakitokea  CCM ni Dk. Evaristo Mtitu,  aliyepata  kura 32 na Ancent Sambala aliyepata  kura 22. Mgombea, Akbar Sanga, alipata kura 21; Rehema Makoga kura nne, Henry Kavina kura tisa, Mussa Mdede kura 48; Mchungaji Samweli  Nyakunga kura mbili na Mwalimu Vitus Lawa akipata kura 14. Kigaila  aliwataka viongozi wa CHADEMA Jimbo la Kalenga kukijenga zaidi chama hicho na kwamba, baada ya kampeni kuanza Wana CHADEMA wilaya zote za Mkoa  wa Iringa  wataingia kazini katika jimbo hilo.
Tanzania Daima

No comments: