Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, February 21, 2014

CHADEMA yahimiza wanachama kugombea uongozi


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Ukonga kimewahimiza wanachama wake kugombea uongozi katika nafasi za udiwani na uenyeviti wa serikali za mitaa katika chaguzi zijazo ili kuwaondolea kero Watanzania. Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa  CHADEMA wa Jimbo la Ukonga, Jumaa Mwipopo,  alipozungumza  na  wanachama  na wapenzi wa chama hicho  katika mkutano wa  kuhimiza uhai wa chama uliofanyika katika viwanja vya Mtaa wa  Markaz, Kata ya Ukonga mwishoni mwa wiki iliyopita.
                  Alisema kuna haja ya serikali  za mitaa za  jimbo  hilo  na Tanzania  kwa ujumla kuongozwa  na CHADEMA,  kwa kuwa  chama  hicho  kipo mstari wa mbele  kupinga  dhuluma  na ufisadi, vitu ambavyo  kwa sasa vinakumbatiwa  na Chama tawala – CCM.
Tanzania Daima

No comments: