Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, February 28, 2014

Mwigulu Nchemba amtusi Dr. Slaa asema "Dr. Slaa ana mapepo saba"

Mh. Mwigulu Nchemba ameshindwa siasa safi na kuendeleza siasa taka. Kwenye clip hii anamtukana katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa, personal.

Mr. Naibu Waziri, this is very very ignorant and personal. We expect you to carry yourself in a professional manner.

PICHA:Ms. Tendega, Heche na Kamanda Mawazo Kampeni Kalenga. Mtoto wa M'kiti wa CCM atia huzuni

 Juu na chini; Meneja wa Kampeni za mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo akiwa amembeba mtoto Zakina Miwela anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Lumuli, ambaye ni mtoto wa kiongozi wa CCM katika kijiji cha Lumuli, anavyoonekana masikini kutona na sare zake za shule kuchanika, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana. 

 Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo, akimwelezea mtoto Zakina Miwela, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Lumuli, ambaye ni mtoto wa kiongozi wa CCM wa kijiji hicho, anavyoonekana bila viatu na sare zake kuchanika, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana.
 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema taifa, John Heche, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Lumuli, wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, Grace Tendega uliofanyika kijijini hapo jana. 
 Makamanda wakielekea kwenye kampeni jimboni Kalenga
Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo na mgombea, GraceTendega, wakizungumza na akinamama wa kijiji cha Lumuli, katika kikao maalumu baada ya mkutano wa kampeni, zilizofanyika kijijini hapo jana.

Kalenga: Moja ya hila ya kukusanya vitambulisho vya kupigia kura

Hii ni moja ya mbinu tulizozibaini ambazo zinatumika kukusanya vitambulisho vya kupigia kura. Tangazo hili la vocha za mbolea ya ruzuku lilikuwa limebandikwa kwenye ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Igula (just a case study), ni hali ambayo iko maeneo mengi jimboni Kalenga tangu uchaguzi ulipotangazwa. Mgombea Tendega Grace amekuwa akilikemea hilo baada ya wananchi kumpatia malalamiko yao.



PICHA: KINACHO ENDELEA JIMBONI KALENGA, CCM NA MABASI, CHADEMA NA WATU


Mkazi wa kijiji cha Tosamaganga, akitembela njiani akiwa ameshikilia bango lenye picha ya mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega, 


Juu na chini Diwani mstaafu kuoitia Chama Cha Mapinduzi tangu mwaka 1982, Thomas Masangula, akiwa ameshika bango lenye picha na mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati wa mkutano wa kampeni za chama hicho, uliofanyika katika kijiji cha Kihanga jana

Moja ya mabasi yaliyokuwa yakisomba wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi, kutika sehemu mbalimbali likiwa njiani kueleka wafuasi hao katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa uliofanyika jana.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Tanangozi, ikiwa ni sehemu ya kampeni za chama hicho za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga juzi.


Moja ya mabasi yaliyokuwa yakisomba wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi, kutika sehemu mbalimbali likiwa njiani kueleka wafuasi hao katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa uliofanyika jana.

Bunge la katiba: Kura ya uwazi (CCM) au siri (taasisi nyingine)


Kwa nini wajumbe wote walio changia kutaka kura ya WAZI ni CCM, lakini wanao taka kura ya SIRI ni wanatoka makundi mbarimbari?

Hawa ni baadhi ya wanaotaka kura ya WAZI

1.Pfr.Anna Tibaijuka, (CCM)
2.Hawa Ghasia, (CCM)
3.Hamis Kigwangala, (CCM)
4.Henry Shekifu, (CCM) 
5.Stephen Wassira, (CCM)
6.Willium Lukuvi (CCM) etc...

Hawa ni baadhi ya waliochangia kutaka KURA YA SIRI

1.Halima Mdee, (CHADEMA)
2.Hashim Rungwe, (NCCR)
3.Mch.Msigwa, (CHADEMA)
4.John Mnyika, (CHADEMA)
5.Esther Bulaya, (CCM)
6.Juma Haji Duni (CUF).
7.Prof.Juma Kapuya (CCM)

So observation ya haraka inaonesha KURA YA SIRI inaungwa mkono na makundi mbalinbali, wapo CHADEMA, CCM, CUF, NCCR, Taasisi za dini, NGOs, vyama vya hiari etc. Lakini KURA YA WAZI inaungwa mkono na kundi moja tu, CCM. We unadhani CCM na kura yao ya wazi watashinda, wakati wameanza kugeukana? Na ni kwa nini CCM peke yao ndo wanataka kura ya wazi? By Mtatiro

Source:Julius S. Mtatiro Facebook Wall


VIDEO: MARIA SARUNGI: BUNGE LA KATIBA: UBABE WA WALIO WENGI NA KATIBA YETU

MARIA SARUNGI: BUNGE LA KATIBA: UBABE WA WALIO WENGI NA KATIBA YETU

   Katika mjadala unaoendelea katika Bunge Maalum la Katiba nilibahatika wiki hii kupata nafasi ya kuchangia na nilizungumzia suala la ubabe wa walio wengi au kwa kiingereza “Tyranny of the Majority”. Nilitumia hoja hii ya msingi kuelezea kwa nini katika mchakato wa kurekebisha rasimu ya katiba tunahitaji kura ziwe za siri. Ila kutokana na ufinyu wa muda sikupata nafasi ya kujieleza kirefu na pia sikuwa na lengo la kuanzisha darasa kwa sababu mi si mwalimu wala haikuwa nafasi yake hapo. Hata hivyo nilimsikia siku inayofuata kaka yangu Peter Serukamba akijaribu kujibu hoja yangu kwa kusema demokrasia ni ya wengi wape. Hii ni hoja ambayo wajumbe wengine pia waliibua. Na imenisikitisha kwamba pamoja na wajumbe hawa tumekusanyika nao katika bunge hili maalum la katiba na hawana uelewa mzuri wa maana pana ya demokrasia. Hawaelewi kwa nini kuna wawakilishi wa asasi zisizo za kiraia na vikundi vya kijamii katika bunge hili maalum la katiba ambao kazi yetu ni kuwasemea watanzania wasiosikika – watoto, akina mama, walemavu, wavuvi na kadhalika. Hawaelewi kwa nini rasimu yetu ya katiba ina haki za binadamu na haki za raia. Kama demokrasia ingekuwa “wengi wape” tu, katiba yetu ingekuwa ina ukurasa chache sana na tungeweza hata kuendelea kuwa na chama kimoja na mgombea mmoja. Lakini sivyo ilivyo na sivyo watanzania tunavyotaka kujenga nchi yetu.

             Hoja yangu ya ubabe wa walio wengi huanzia kabla kura hazijapigwa na baada ya kura kupigwa. Umuhimu wa kura ya siri ni kuwalinda wale ambao wanaweza kutishiwa kwa njia moja ama nyingine yaani “protection from intimidation”. Lakini pia kuna hoja ya kuwa ni haki ya msingi ya kila mtu yaani haki ya uhuru wa mawazo na maoni. Kura ya siri inampa uhuru huu kila mtu. Lakini kwa mwonekano wangu hoja zaidi ni kama wataalam wengi wanavyoshauri kuwa kura ya siri ni muhimu pale ambapo uwezekano wa kutishiwa au kushurutishwa upo. Katika mazingira kama haya basi ni njia mwafaka wa kupata maamuzi. Bila kupoteza muda ningependa kurudi kwenye hoja wa “walio wengi” kwani hata dhana hii inabidi tuijadili zaidi.

          Kusema wingi wa kura pekee ndo demokrasia ni mwonekano mfinyu. Hebu nifafanue kidogo kwa faida ya wale ambao uelewa wao haujapanuka kwa nini nimetoa tahadhari aliyoitoa James Madison na John Adams – moja wa vinara waliotunga katiba ya Marekani - kuhusu ubabe wa walio wengi. Hoja ya “walio wengi” (majority) si lazima iwe hoja yenye maslahi ya taifa kutokana na ubinadamu wetu. Na John Adams alifafanua vyema maslahi haya kuwa yanaweza kuwa maslahi ya familia zao, vitongoji vyao au vyama vyao. Hivyo alisihi kuwa kuna haja ya kuweka vifungu katika katiba itakayotetea mfumo wa haki, kuwalazimu wote kuheshimu maslahi ya pamoja na ya taifa dhidi ya maslahi binafsi au ya kichama:

“If a majority are capable of preferring their own private interest, or that of their families, counties, and party, to that of the nation collectively, some provision must be made in the constitution, in favor of justice, to compel all to respect the common right, the public good, the universal law, in preference to all private and partial considerations”

        Hivyo basi John Adams alisisitiza kuwa vifungu hivi vya katiba yaani Bill of Rights ndivyo vitakavyomlinda mtu binafsi kutokana na kile kinachoitwa ubabe wa walio wengi. Haki hizi ni pamoja na uhuru wa maoni, uhuru wa kupata hifadhi, uhuru wa dini na kadhalika. Katika chapisho la “Federalist papers” maandiko yaliyokusanywa ya wale vinara walioshiriki kutunga katiba ya Marekani, James Madison pia alionya na kutoa hali halisi iliyokuwepo wakati huo katika siasa za Marekani. Alieleza ni jinsi gani wananchi wengi wanalalamika kuwa serikali haziaminiki, na maslahi ya umma yanawekwa pembeni kutokana na ushindani wa vyama vya kisiasa; na vitu vinaamuliwa si kwa kufuata misingi ya haki na kulinda walio wachache au wasio na sauti (minority), lakini kwa kufuata nguvu kubwa ya walio wengi wenye maslahi binafsi.

“Complaints are everywhere heard from our most considerate and virtuous citizens, equally the friends of public and private faith, and of public and personal liberty, that our governments are too unstable, that the public good is disregarded in the conflicts of rival parties, and that measures are too often decided, not according to the rules of justice and the rights of the minor party, but by the superior force of an interested and overbearing majority.”

         Na ndiyo maana hata James Madison alizungumzia umuhimu wa vifungu vya katiba vitakavyolinda haki ya mtu binafsi yaani Bill of Rights. Ni dhahiri kuwa hao “walio wengi” leo, kuna siku lazima watakimbilia kutaka kulinda haki zao kwa mfano haki ile ya “kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake na familia yake na nyumbani kwake, kutoteswa au kudhalilishwa na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake binafsi”. Kila mmoja wa “walio wengi” atapigia kelele haki zake binafsi kwa sababu kuna uwezekano mlio wengi mkawa wachache. Historia ina mifano ya kutosha.

       Hivyo basi huwa napenda kusema kuwa historia ina mengi ya kutufundisha na wala tusidhani kuwa eti tumevumbua sisi demokrasia au suala la katiba. Kama tumeamua kuwa Tanzania iwe nchi inayoheshimu demokrasia basi tufuate misingi yake na tujikite kuelewa vyema misingi hii. Ubabe wa “walio wengi” inategemea hao walio wengi ni kina nani na katika mazingira gani. Je “walio wengi” ndani ya chombo maalum kinachoandika katiba ndiyo kweli “walio wengi” Tanzania? Je hawa “walio wengi” wana wingi wa nini na je tunaweza kuwaamini kuwa watakuwa na wingi huo siku zote? Je tunaweza kusema kwa uhakika kuwa “walio wengi” wanasukumwa na maslahi ya umma na kila mmoja wao ataheshimu siku zote msingi wa haki? Jibu ni hapana. Na si kwamba hawa “walio wengi” sasa ni wabaya sana kuliko wengine lakini ukweli ni kuwa kama nilivyowahi kusema katika siasa hakuna malaika wala shetani. Hivyo kama mchakato wa sasa wa katiba mpya iko katika chombo ambacho kimetawaliwa na wanasiasa basi tujue hapo tunatakiwa tuwe makini sana. Tujikite kutetea haki za wote na tuweke misingi itakayohakikisha kuwa maslahi binafsi au ya kichama hayatawali.

       Sasa kwa nini niliibua hoja hii ya ubabe wa walio wengi? Nililiibua kwa sababu kabla hata hatujaanza mjadala kuhusu rasimu ya katiba, tukiwa bado tunajadili rasimu ya kanuni zitakazotuendesha, ubabe huu umeonekana na ni hatari kwa mustakabli wa taifa. Kwani inaashiria kuwa ubabe huu utaendelezwa mpaka kwenye mijadala ya hapo mbele kuhusu rasimu ya katiba bila kuelewa vyema kilichotuleta pamoja hapa Dodoma. Hivyo nasema walio wengi wasijitetee na wasitake kutushawishi kuwa ni malaika, na mimi binafsi pamoja na wengine hata tusipokuwa na mitazamo iliyofanana nao tusitake kuwafanya “walio wengi” ni waovu, ila tutambue hali halisi na tufuate misingi ya demokrasia.

         Kwa kumnukuu Edmund Burke mwanasiasa na mwanafalsafa wa Uingereza: “the greater the power, the more dangerous the abuse” yaani jinsi nguvu inavyozidi kuwa kubwa ndivyo dhuluma inaongezeka. Basi nguvu ya walio wengi isiwe ya ubabe na dhuluma, bali iwe ni nguvu ya kweli na yenye kujitambua inayotaka kujenga utaifa na kujali raia wote na haki zao. Kama msanii wa kifaransa, Paul Cezanne alivyosema “the awareness of our strength makes us modest” yaani kutambua nguvu tuliyo nayo hutufanya tuwe wa kawaida au kujishusha. Mtu mwenye nguvu ya kweli na anayejitambua kamwe hawezi kuwa mbabe na siku zote hutafuta njia ya kuwasaidia wasio na nguvu. Si kwa sababu ya huruma, lakini kwa sababu anaelewa nguvu yake imetokana na nini.  Hawa “walio wengi” leo watakapopata jibu kuwa nguvu yao imetokea wapi wataelewa kuwa misingi hii ya demokrasia na utaratibu tunajijengea sote kwa sababu hata kama si leo au kesho lakini hatimaye mpanda ngazi hushuka.


Wabunge wawili CCM wajilipua

        Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Ester Bulaya akichangia hoja juu kuhusu Kanuni za Bunge, Dodoma jana. Bulaya, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), aliunga mkono hoja ya kura za siri.  Picha na Emmanuel Herman 
          Wajumbe watatu wa Bunge la Katiba ambao ni wabunge wa CCM wametofautiana na msimamo wa chama chao kwa kuunga mkono kura ya siri itumike kuamua ibara za Rasimu ya Katiba. Hilo lilitokea jana katika mjadala mkali baina ya wajumbe kuhusu ama matumizi ya kura za siri yatumike au kura za wazi. Katika mjadala huo ulioonyesha mgawanyiko wa wazi, wajumbe wengi wanaotokana CCM na ambao wamekuwa wakipigania kura za wazi, walionekana kuwazidi kwa wingi wale wanaotaka kura za siri. Wajumbe wa CCM ambao ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muunganom– Esther Bulaya na Profesa Juma Kapuya walijitoa mhanga na kueleza bayana kuwa hawako tayari kuona demokrasia ikikandamizwa kwa kulazimishwa kupiga kura za wazi. Akishangiliwa kwa nguvu, Bulaya alisisitiza kuwa hayuko tayari kulazimishwa kupiga kura ya wazi huku akijua kuwa utaratibu huo unamnyima uhuru wake. “Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko. Ni lini na wapi maamuzi magumu kama haya yalifanyika?” Alihoji mbunge huyo wa Viti Maalumu.

     Bulaya alisema hakuna sheria inayomtaka mtu kushurutishwa kufanya uamuzi na kwamba kumtaka atoe sauti ya juu katika kura za wazi, ni kumlazimisha kufanya kinyume na matakwa yake. Alisema kamwe hawezi kuuza uzalendo wake kwa kupiga kura za wazi na kwamba atapimwa kwa utashi wake kuhusu kile anachokiamini. Kwa upande wake, Profesa Kapuya alisema namna nzuri ya kumpa uhuru mpiga kura, ni kutomshurutisha ili afuate matakwa ya wengine. Alisema kura za siri ndizo zitakazowaimarisha wajumbe na kwamba kinyume chake, kura za wazi zitawagawa na hatimaye kutoka bungeni wakiwa vipande vipande. Kwa upande wake, Anna Kilango Malecela aliunga mkono ‘kiaina’ kura ya siri akisema alimsikiliza Profesa Ibrahim Lipumba kwa karibu saa nzima kupitia Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC), akamshawishi kutokana na hoja alizozitoa. Alisema kwa kuwa suala hilo limezua mvutano mkubwa katika bunge hilo, ni bora likaamuliwa kwa kupigiwa kura ya siri.
Wajumbe wengine

Thursday, February 27, 2014

Rasimu Ya Pili Ya Kanuni Za Bunge Maalum Toleo La 2014

Kura ya wazi Rasimu ya Katiba italeta Uhasama!.

Na Bryceson Mathias

HATULITAKI Kundi dogo la watu wenye nguvu ya Fedha na matakwa yao binafsi miongoni mwa wajumbe wa Bunge la katiba, wanaopinga kura ya siri wakitaka iwepo kura ya wazi bungeni humo, ambayo tuna imani kubwa kwa vyovyote italeta Uhasama.

Tumekuwa tukishuhudia Viongozi wa Serikali na Wabunge wao, wakijifungia kwenye kumbi kuweka misimamo na maagizo ya vyama vyao! Ningetoa rai tusingependa kuona kura ya wazi yenye majanga, visa, vifo na umwagaji damu, inaidhinishwa na wabunge wa rasimu hii.
Ikumbukwe; Tumechoshwa kuona damu zisizo na hatia zinamwagika kila mara kwa sababu ya mashinikizo ya wana siasa wachache wenye uroho na ubinafsi wa madaraka, ambao kila siku wanapigia upatu waendelee kuwa na nyadhifu na vyeo vya kutoa Kafara.

Kutoka na uzoefu tuliouona nyakati za vikao vya Bunge la Muungano, ambapo hupiga kura za ndiyo na hapana ambazo kwa sehemu kubwa huwa hazina usahihi kutokana na kuamuliwa kwa udhaifu wa wingi wa sauti za watu, historia ya Bunge hili Maalum la Katiba si la ulegelege huo.

Tuna ushahidi; Iwapo utaratibu wa kura ya wazi utatumika kwenye maamuzi ya Bunge Maalum, utaminya haki na kuwapa haki watu wenye uwezo wa kushinikiza watu wapige kura kwa uoga na mashinikizo ya fedha au vitisho.

Hatuipendi kura ya wazi kwa sababu, inaweza kumpa fursa Mwenyekiti wa Bunge hilo asiyekuwa makini, kuunyima au kuupatia upande wenye sauti kubwa ya fedha kujibu hata kama ni wachache,  na ukapate kura ambazo hata kama zilikuwa za watu wengi lakini hawana sauti ya hela.

Kura ya wazi inamkaba mpigaji kutokuwa na uhuru, na kwamba anaweza kubadili mawazo na makusudi aliyokuwa nayo kutokana na kuona anayehusika na kitu wanachokipigia kura, hivyo kwa Fadhira, Huruma au Woga wa kununiana na kueleweka vibaya, akalazimika kupigia upande wake.

Kura ya wazi ina mwanya mkubwa  wa kupenyeza Rushwa, ambapo ikitokea wakati wa kupiga kwa wazi kwa maana ya kunyosha vidole,  kusimama nyuma ya mtu au kujibu ndiyo au hapana kwa kuitwa majina; ni dhahiri kutakuwa na uhasama na visasi vyenye maafa baadaye, kama mtu ataacha kumchagua.

Rai hii inafuatia kuanza kujitokeza vikao hivyo (Part Cocas)  kwa vyama katika kumbi zilizozoeleka wakati wa Bunge la Kawaida la Muungano, ambapo kwa Bunge hili Maalum, tunahoji, wajumbe wa Taasisi wasiokuwa na kumbi watakutana wapi? Kwa nini Wabunge hawajui kuwa hili si Bunge la vikao  vya Muungano?

Tulikuwa tunatarajia kama kunakuwa na vikao vya kujadili mustakabali wa Rasimu namna hiyo, basi wabunge wote zaidi ya 600 wangekaa pamoja na kujadiliana mapungufu na nyongeza nzuri za maandiko ya rasimu hiyo, lakini vyama vinapojigawa kwa itikadi zake haituingii akilini.

Migawanyo hiyo kama inafanywa na Serikali au Viongozi wake, ni kinyume cha Sheria ya Rasimu hiyo, maana jopo hilo lililoteuliwa, linatakiwa liwe pamoja kama timu kujadili mustakabali wa rasimu hiyo bila kuwa vipande vipande vya mijadala vinavyofanywa hivi sasa kwa kujifungia kwenye kumbi au vyumba.

Kama mipaka na migawanyo hiyo itaendelea, ni dhahiri mwisho wa yote tutakuwa na  Katiba ya  mashinikizo iliyojaa ubabaishaji ambayo itakuwa Janga na watanzania wategemee kulia kwa mateso yatakayotokana na Katiba Ubabishaji kwa mika Mingi, huku Kodi ya wananchi ikiwa imepotea.

Picha: Kampeni jimbo la Kalenga, Iringa


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrfod Slaa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kiwele katika mkutano wa kampeni wa uchaguzo mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa juzi.
Juu na chini Mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kiwele katika mkutano wa kampeni juzi.

Wananchi wa kijiji cha Kiwele wakiitikia moja ya salama za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati wa mkutano wa kampeni za chama hicho za uchaguzo mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa juzi.
Mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega akisalimiana na mmoja wa wazee wa kijiji cha Kiwele, baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo juzi.








Kazi na dawa, LUNCH TIME!

Wednesday, February 26, 2014

Mnyika ataka uwazi ufuatiliaji posho


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, John Mnyika (pichani), amemtaka Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Ameir Pandu Kificho, kuwasilisha taarifa ya kazi zilizofanywa na kamati ya kufuatilia posho na kanuni ili iwe wazi kwa wajumbe na jamii. Kadhalika, alisema usiri, udhaifu na uzushi uondolewe mjadala ni Katiba mpya na siyo posho.

Katika taarifa yake, alisema usiri na udhaifu wa uongozi wa Bunge katika kutoa taarifa na uzushi wa baadhi ya viongozi au watendaji wa serikali na baadhi ya wajumbe umesababisha majalada wa Rasimu ya Katiba kubadilika na kuwa posho.

Alisema ili kulirudisha Bunge Maalum katika mkondo sahihi kwa kujadili kanuni na rasimu ni vyema Katibu wa Bunge na Baraza la Wawakilishi watoe taarifa ya ziada ya kazi ambazo kamati za muda za uongozi na kanuni za kumshauri zimefanya.

“Makatibu wasipofanya hivyo, Mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho, atumie ufunguzi wa semina ya kanuni za Bunge kueleza kazi kubwa iliyofanywa na namna ambavyo kwa ukubwa wa kazi muda umeongezwa na muda wa ziada wa kuwasilisha kanuni zilizofanyiwa marekebisho,” alisema.

Kitomory S./ Ippmedia-Nipashe