Tawi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) DMV, USA, tumepigwa
butwaa na mshituko mkubwa kupokea habari ya kifo cha dada yetu, Zainabu Buzohela, kilicho tokea January 4, 2014. Tawi la CHADEMA DMV tunatuma salamu za
rambirambi kwa mume wa marehemu Ndg. Dullah, dada mdogo wa marehemu Bi. Ngalu,
familia , ndugu jamaa na marafiki wa marehemu Zainabu.
Tawi la CHADEMA, DMV, tupo pamoja na ndugu, jamaa, marafiki wa
marehemu Zainabu na waTanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza
dada yetu.
KAZI YA MOLA HAINA
MAKOSA
No comments:
Post a Comment