KAMBI YA CCM GREEN GUARD,
CHIMALA, MBEYA, YAVUJISHA RIRI
Kila
kilichokua kinaendelea katika kambi ya CCM Chimala tulikua na watu wetu.
Kamanda Beni wa mbeya mjini alifanikiwa kuingiza watu kumi;CHADEMA Chimala
iliingiza makachero watatu 3.
Kuna kadi za
CHADEMA 200 ambazo zilitoka kwa Braison Mwasimba aliyefukuzwa CHADEMA ( alikuwa
katibu wa tawi CHADEMA Nzovwe, Mbeya) amekabidhi hizo kadi kwa Gunza wa CCM;
huyu ni mwalimu wa Wigamba sekondari (Isanga) na alikuwepo pia katika mafunzo
ya Green Guard Chimala. Kadi hizo za CHADEMA wanapanga kuwapa watu siku ya
maazimisho ya kuzaliwa CCM ili wazirudishe kwa J. Kikwete. Mpango huu mahusui
ni kutaka kumuonyesha Kikwete kuwa CCM inakubalika Mbeya. Hii ni miongoni mwa
agenda yao CCM.
CCM
wamewafukuza watu kumi na tano (15) kutoka kwenye hiyo kambi, ambao nao
walikuwa ni “source” wa hii habari baada ya kupigwa chini. Kati ya walio
fukuzwa ni kuwa waligundulika wanatoa siri na wengine walifanya mgomo kutokana
na kuahidiwa malipo ya Tsh 10,000/= kwa siku na badala yake kuwa wanalipwa
2,000/= kwa siku.
Mambo
yaliendelea kuwa mabaya baada ya chakula kuisha kambini. Ndipo mwenyekiti wa
CCM wilaya, Ndg Mathayo Mwangomo alipo amua kumpigia simu mkuu wa magereza
wilayani, Rujewa, na kuomba chakula. Mkuu wa magereza ali mgombeza na kumwambia
kuwa usirudie kunipigia tena simu kwani shughuri za chama na magereza
haziingiliani. Baada ya chakula kuisha ikabidi waanze kutumia pesa ya posho
kununua mahindi na viazi. Hapo ndipo yale malipo ya 2,000/= yakakata na kukawa
na mtafaruku kambini.
Green guard
walianzisha mgomo na kusema kuwa wanafanya mazoezi magumu hawawezi kurishwa
viazi na wanadai fedha zao. Grean gurad waliandamana na kwenda kituo cha polisi
Chimala; walikuwa vijana kama 280. Wakaambiwa waje na viongozi. Baada ya
viongozi kuja wali ongea na kuyamaliza; kesho yake wakapewa 10,000/= kila
mmoja. Kiongozi aliye anzaisha maandamano akapigwa chini, wakati huo vijana
sita washafukuzwa.
Makachero wetu
wamefanikiwa kurekodi maongozi ya makubaliano ya pesa. Pia wamerekodi walivyo
kuwa wanafanya makubariano ya hizo kadi 200 hapo kambini na Ndg Mwasimba.
Wamerekodi hadi maongezi ya kijana walivyo kuwa wakimfukuza na kumnyima nauli;
huyo kijana anatokea Mbeya. Record tuliyo nayo ni audio ambayo itatolewa muda
muafaka utakapo fika.
Kijana mmoja
msamalia mwema wa Chimala ambaye anaitwa Rodi; ni kamanda wa CHADEMA aliwaone
huruma vijana walio fukuzwa na bila kupewa nauli kwani walifukuzwa usiku na
hawakuwa na mahala pa kulala. Alijitolea kuwarudisha mbeya mjini kwa gari lake.
Green Guard
imeondoka leo, Jumamosi, February 1, 2014 kuelekea Mbeya mjini kwaajiri ya
sherehe za kuzaliwa CCM.
On other note;
Mathayo Mwangomo (Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Mbarali) amekuwa akiwatishia watu
kuwa yeye ni serikali na atawaweka ndani. Alikutana na mwenyekiti wa CHADEMA
Chimala ambaye alimchana na kumwambia yeye ni mwenyekiti wa CCM wilaya na sio
serikali.
TAKE
AWAY: KUNA KADI ZA CHADEMA 200 ZITARUDISHWA SIKU YA KUZALIWA CCM MBEYA.
HIZI NI KADI AMBAZO ALIYE KUWA KATIBU WA CHADEMA, NZOVYWE , MBEYA, ALIKUWA
NAZO. KADI HIZO HAKUZIREJESHA BAADA YA KUFUKUZWA UONGOZI
WE REPORT, YOU DECIDE
No comments:
Post a Comment