![]() |
Joseph Golliama |
Nia na Lengo la
kila chama cha siasa ni kushika Dola ili kiweze kujenga Taifa na kusimamia
Ujenzi wa Taifa na kufanya wananchi wa makundi yote wapate maisha Bora na Taifa
Zima lipate ustawi na maendeleo endelevu, katika kupambana kufanikisha nia na
lengo la kushika Dola kila chama kina jukumu la kuhakikisha kinatumia makosa ya
serikali ya chama kilichopo madarakani kuwahahakikishia wananchi kama chenyewe
kitapewa lidhaa ya kushika dola basi kitafanya mazuri kwa manufaa ya Taifa
kuliko serikali iliyopo madarakani. mambo muhimu ambayo kila chama kinapaswa
kuyatazama na kuyakosoa kwa serikali iliyopo madarakani ni haya
1. Serikali
iliyopo madarakani inapaswa kuhakikisha Taifa linakuwa na Sauti moja ya
kuisikiliza na kama Taifa halina Sauti moja ya kuisikiliza hilo ni jambo la
kuihoji serikali iliyopo madarani kwani ni wajibu wake. Inapofika wakati
wananchi kama hawajui sauti ya kuisikiliza na wanajiuliza hivi tuisikilize
sauti ya viongozi wa dini zetu au tusikilize sauti ya viongozi wa vyama vyetu
au tusikilize sauti ya viongozi wa makabila yetu au tuisikilize sauti ya
serikali hii inaonyesha Taifa linatatizo kubwa haliijui ni sauti ipi ya
kuisikiliza.
2. Serikali
iliyopo madarakani inapaswa kuhakikisha Taifa linakuwa na mwelekeo mmoja wa
kuufuata na kama Taifa halina mwelekeo mmoja wa kuufuata hilo ni jambo la
kuihoji Serikali iliyopo madarakani kwani ni wajibu wake.Taifa lisilo na
mwelekeo mmoja ni Taifa lililo njia panda lisilojua kwa kwenda
3. Serikali
iliyopo madarakani inapaswa kuhakikisha Taifa linakuwa na Muafaka wa kitaifa wa
ujenzi wake yaani muafaka wa makundi yote ya wananchi wa aina ya Taifa
tunalotaka kulijenga litakalohakikishia makundi yote ya wananchi ustawi na
maendeleo endelevu, muafaka wa ujenzi wa Taifa ndio pekee uwezao kuyafanya
makundi yote ya wananchi kuwa na amani katikati yao kama haupo amani miongoni
mwa makundi hayo inakuwa adimu.ili kuepuka Taifa kugawanyika kwa misingi ya
makundi ya wananchi ni lazima pawepo muafaka wa makundi yote wa ujenzi wa Taifa
laasivyo Taifa litagawanyika kwa misingi ya Dini,vyama vya siasa,matabaka ya
maisha,makabila,jinsia,rika nk
4. Serikali
iliyopo madarakani inapaswa kuhakikisha Taifa linakuwa na Umoja wa upendo ndani
yake, umoja ni ile hali ya makundi ya wananchi kupendana na kuthaminiana na
kujaliana hivyo serikali inawajibu wa kuwaongoza wananchi kuacha tabia
zinazihatarisha umoja wao na umoja wa Taifa kwa ujumla wake,tabia hizi
zinapaswa kupigwa vita na serikali ndani ya Taifa ili umoja wa Taifa uimalike,
tabia za makundi mbalimbali kuwa na chuki,uadui,fitina,faraka,uzushi,ugomvi,ufisadi,ulevi,uchu,Wivu,ujambazi,Uwizi,tamaa
mbaya, usengenyaji,
manung'uniko,ushoga,uuaji,ubakaji,uonevu,ukatili,ujeuri,uchokozi,
uzembe,uzinzi,uasherati,umalaya,ugaidi,uchafu,uchawi,roho mbaya,ulawiti,hasira,
5. Serikali
iliyopo madarani inapaswa kuhakikisha Taifa linakuwa na mawasiliao ya haki
ndani yake, mawasiliano ni ile hali ya makundi ya wananchi kuaminiana na kila
kundi kuona kundi lingine lina haki ndani ya Taifa, hivyo serikali inapaswa
kujenga mawasiliano kwa kuongoza makundi yote ya wananchi kubomoa katikati yao
tabia za
kukataana,kuhukumiana,ukabila,unyonyaji,dharau,udini,udhehebu,uzuluraji,ubinafsi,madeni,kisasi,umaskini,ujinga,laana,magonjwa,kupenda
fedha,kupenda mali,kupenda anasa,kupenda sifa,ubahiri,Rushwa, ukimbizi wa aina
zote,kukata tamaa,kujikweza, kukosa shukrani,Dhuluma,Talaka zisizo za
msingi,Vita, upendeleo,Ukanda,umaeneo,Uchama, na kila kisicho haki serikali
inapaswa kuongoza wananchi kukikataa na kukiacha
Nguvu zote na
mamlaka zote ambazo serikali inazo inapaswa kuzitumia kufanya hayo mambo matano
na kusimamia Taifa kuhakikisha milele linabaki kuwa na Sauti moja ya
kuisikiliza linakuwa na mwelekeo mmoja wa kuufuata, linakuwa na amani, umoja wa
upendo na mawasiliano ya haki hapo TAIFA letu litaanza kusonga mbele kuelekea
ustawi na maendeleo endelevu
Kama serikali
iliyopo madarakani haifanya hayo vyama vya siasa vinapaswa viitumie hali hiyo
ya serikali kuwa dhaifu katika kutimiza maslahi ya TAIFA Kuwahakikishia
wananchi kwamba wao wakipewa nafasi ya kuunda serikali watatimiza hayo kwa kutumia
nguvu na mamlaka ya raslimali za Taifa letu
Ushauri 1;
Chama chenye serikali iliyopo madarani kinapaswa kuisimamia serikali
kuhakikisha kinafanya haya ninayoyashauri ili kiendelee kupewa fulsa ya kushika
dola otherwise ipo siku kitajilaumu kwa kushindwa kutumia fulsa adimu ambayo
wananchi walikipa
Ushauri 2;
Vyama vinavyotaka kushika Dola angalieni udhaifu wa serikali katika kutumia
mambo hayo kwani mkiwahahakikishia wananchi wa makundi yote kuwa mtaunda
serikali itakayofanya Taifa letu kuwa na sauti moja ya kuisikiliza, mwelekeo
mmoja wa kuufuata, amani, umoja wa upendo na mawasiliano ya haki naamini Mungu
atakuwa nanyi na ipo siku kama dhamiri yenu ni ya kweli Mungu atawapa
mkitakacho
Nawasilisha
mchango wangu wa mawazo kwenu wananchi wenzangu
Joseph
Goliama
No comments:
Post a Comment