Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, October 29, 2013

Wahariri waisulubu serikali kuteswa Kibanda

   JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limeishambulia serikali na Jeshi la Polisi kutokana na ukimya wake katika suala la kushambuliwa na kusababishiwa ulemavu wa kudumu kwa Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006), Absalom Kibanda. Akisoma maazimio ya mkutano mkuu wa jukwaa hilo uliofanyika wiki iliyopita mkoani Iringa, Katibu wa TEF, Nevile Meena, alisema ukimya huo ni hatari na unaweza kutumiwa na watu wabaya kufanya unyama kwa waandishi. Katika mkutano huo ambao mada kuu ilikuwa “usalama wa waandishi wa habari nchini Tanzania” wakirejea matukio mawili makuu ya mauaji ya Daud Mwangosi na kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa Kibanda, Meena alisema yanathibitisha kutetereka kwa usalama wa waandishi wa habari nchini. Alisema usalama dhidi ya waandishi wa habari ni suala nyeti na kwa kuzingatia yale yaliyowapata wenzao, watahakikisha wanafanya kila linalowezekana matukio hayo kuwa ya mwisho kuwapata waandishi.

         “Tungependa kuona wahusika wanakamatwa na kufikishwa mahakamani, lakini mpaka sasa ni kimya, si viongozi wa serikali wala ndani ya Jeshi la Polisi wanaolizungumzia hili, na hali hii inaweza kuwa kichocheo cha wanaotekeleza matendo hayo,” alisema Meena. Meena alisema kuwa usalama wa waandishi wa habari hauwezi kutenganishwa na mfumo wa sheria unaosimamia tasnia ya habari, na kwa maana hiyo wameazimia kupigania kuwapo kwa sheria mahsusi kwa ajili ya kuwalinda waandishi wa habari kutokana na asili ya kazi zao na mazingira ya hatari wanayofanyia kazi. “Katika mazingira ya sasa, kutoa taarifa hizo hadharani kunaweza kumpeleka mwandishi na chanzo chake jela, tunataka sheria ya kuwalinda waandishi kwani kwa hii ya sasa mahakama inaruhusiwa kulazimisha kutajwa kwa vyanzo,” alisema Meena.

Source: Khamis A. ( Oct. 2013).Wahariri waisulubu serikali kuteswa Kibanda. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: