Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, October 27, 2013

PICHA: UFUNGUZI TAWI LA CHADEMA OHIO, USA, OCT 26. 2013

Kutoka kushoto: Katibu muenezi Ohio, Rehema Mwenda, Katibu mkuu DMV, Liberatus Mwangombe "Libe", Katibu mkuu Ohio, Helene Ongara, Mwenyekiti Ohio, Salva Muhaya na Mwenyekiti DMV Kalley Pandukizi wakiingia ukumbini

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kimefungua rasmi Tawi lake katika Jimbo la Ohio Marekani Siku ya Jumamosi tarehe 26 Oktoba 2013. Sherehe hizo zilihudhuriwa na Wakazi mbalimbali wa Jimbo la Ohio na Majimbo mengine ya Jirani kama Alabama. Mgeni rasmi katika Sherehe hizo alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Washinton DC, Ndugu Kalley Pandukizialiyeambatana na Katibu wa Chadema Washington DC Liberatus Mwang’ombe na Viongozi wengine wa Chadema DMV. Tukio hilo la ufunguzi lilianza kwa Mwenyekiti wa Chadema wa Ohio Ndugu Salva Muhaya kuongea historia fupi ya Kuanzishwa kwa Tawi hilo. 

Baadaye lilifuata tukio la kukata utepe kama ishara ya kufungua tawi hilo rasmi, lililofuatiwa na tukio la kukata keki kama ishara ya kuanza sherehe za Ufunguzi rasmi. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na mmoja wa Wanachama Wakongwe kabisa wa Chadema Mzee Gervas Kavishe aliyejiunga Rasmi Chadema kama mwanachama tangu mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ulipoanza. Akizungumza katika Sherehe hizo Mgeni rasmi Ndugu Kalley Pandukizi aliwasisitiza Watanzania wanaoishi  Diaspora kujiunga na Chadema ili kuleta Ukombozi kwa Mtanzania aliyekatishwa tamaa na hali mbaya ya Maisha. Naye Katibu wa Tawi la Chadema Washington DC, Ndugu Liberatus Mwang’ombe aliwasisitiza Watanzania wanaoishi Diaspora Kujua umuhimu wa kutoa Michango yao ya Hali na Mali katika Harakati hizi za Kulikomboa Taifa, Kwani wanaoathirika na hali mbaya ya Maisha ni Ndugu zetu hivyo lazima tuguswe na hilo na tutafute namna ya kuwasaidia kwa kila hali. 
























Kada wa CCM, benjamini Mwaipaja, naye alikuwepo kubadirishana mawazo

Wageni waalikwa


1 comment:

Dennis Mzelela said...

I like it that way, keep it up up up up mpaka kieleweke