CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema suala la muungano na serikali tatu ni muhimu ili kurahisisha utendaji kazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Tanzania Bara. Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa juzi na Katibu wa Jumuia ya Wanawake wa CUF Taifa, Nuru Bafadhiri Awadh, katika hafla ya ufunguzi wa tawi jipya la chama hicho la New Mauzi lililofunguliwa kata ya Duga. “Serikali tatu zinahitajika katika kipindi hiki kwani zitaharakisha utendaji kazi kwa pande zote mbili badala ya sasa ambapo kumekuwa ni mzigo kwa Rais wa Jamhuri kwa kufanyakazi za Zanzibar ambazo zingemalizwa na Wazanzibar wenyewe,” alisema Awadh.
Alisema chama hicho ndicho kilikuwa cha kwanza kupendekeza kuwepo kwa serikali tatu na kudai Katiba mpya ili kuwepo kwa uhalisia wa Utanganyika. Wakati huohuo, Diwani wa Mwanzange, Rashid Jumbe, alisema suala la wananchi kukimbilia kwa waganga wa kienyeji linatokana na huduma duni zinazotolewa katika zahanati na hospitali za umma. “Tusimtafute mchawi; ongezeko la wananchi kwenda kupata matibabu kwa waganga wa jadi linachangiwa na huduma mbovu zinazotolewa katika hospitali za serikali,” alisema Jumbe.
Source: Kilindi E. ( September 2013). CUF: Serikali tatu muhimu. Retrieved from Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment