Mansoor Yussuf Hamid |
Dk. Shein ndiye aliyeongoza
kikao cha Kamati ya Maadili, huku wajumbe wakiwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Mohamed Hija, Mbaruk Rashid Omari na Makamu wa Pili wa
Rais, Balozi Seif Ali Idd.
Chanzo hicho kutoka ndani ya CCM Zanzibar, kilisema
tuhuma za Mansoor zilizowasilishwa zilikuwa tatu, huku ya kwanza ikiwa ni
kushindwa kusimamia malengo, madhumuni na masharti ya chama.
Aidha, Mansoor
anadaiwa kutokusimamia wajibu wa mwanachama kwa kukiuka maadili ya kiongozi wa
CCM, kwa kukiuka Ilani ya chama hicho ya mwaka 2010.
Hata hivyo, ilielezwa
kuwa suala la kufukuzwa uanachama kwa mwakilishi huyo lilizua mjadala mzito
katika kikao cha jana, lakini baadaye wajumbe walikubaliana kwa kauli moja
kufukuzwa kwake.
Mansoor amekuwa miongoni mwa Wazanzibari walio katika safu ya
mbele kutetea muundo wa Muungano utakaoipa Zanzibar mamlaka kamili ya dola.
Chanzo
hicho kilizidi kusema kuwa suala la mwakilishi huyo kutakiwa kuwasilisha
utetezi dhidi ya tuhuma zake, lilianzia katika kikao cha CCM Mkoa wa Mjini
Magharibi ambapo alisema kama kufungwa afungwe lakini atasimamia Muungano wa
mkataba pamoja na mamlaka kamili.
“Katika kikao cha mkoa alitoa utetezi wake
na kusema kama kufungwa afungwe, kama kunyongwa anyongwe na kama kufukuzwa afukuzwe,
lakini anataka Serikali ya mkataba.
“Wakati anatoa utetezi wake, Mansoor,
alikuwa anatumia nakala moja ya gazeti la wiki la Julai 26, mwaka huu na
kumtuhumu Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, kuwa naye anavunja
Katiba ya CCM,” kilisema chanzo hicho.
Kutokana na misimamo yake, Mansoor,
anaaminika zaidi kwa Wazanzibari hususani wale wanaoamini katika Muungano wa
mkataba pamoja na madaraka kamili ya dola ya Zanzibar.
MTANZANIA ilipomtafuta
Msemaji wa CCM upande wa Zanzibar, Waride Bakari Jabu, atoe ufafanuzi wa suala
hilo, alisema yupo katika kikao.
“Kwa sasa siwezi kusema jambo lolote
mwanangu, nafikiri unasikia sauti za wajumbe wakizungumza, nipo katika kikao na
siwezi kusema jambo lolote kwa sasa,” alijibu kwa kifupi Waride.
Historia yake
Katika uchaguzi wa mwaka 2005, Mansoor, alichaguliwa kuwa Mwakilishi wa
Kiembesamaki kupitia CCM, nafasi ambayo amedumu nayo hadi sasa.
Pia ni
mwanachama wa CCM aliyewahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC), Halmashauri Kuu
(NEC) na Mweka Hazina wa CCM upande wa Zanzibar kati ya mwaka 2002 hadi mwaka
2012.
Nje ya CCM, ameshika nyadhifa mbalimbali za uwaziri katika Baraza la
Mawaziri la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
Mwaka 2000 hadi mwaka
2004, alikuwa Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, na kati ya mwaka
2004 hadi mwaka 2010 alikuwa waziri kamili katika wizara hiyo na baadaye mwaka
2010 hadi mwaka 2012, alikuwa Waziri wa Kilimo na Rasilimali.
Aidha, alihudumu
kama mjumbe wa Baraza la Biashara la Zanzibar kati ya mwaka 2002 hadi 2012.
Kutokana
na misimamo yake ndani na nje ya chama na Serikali, Oktoba 15, 2012, Dk. Shein
ilimlazimu kufuta uteuzi wake kwa Mansoor kuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi.
Mansoor
ni mwanasiasa na mfanyabiashara aliyezaliwa Novemba 3, 1967 kisiwani Unguja.
Alisoma masomo yake ya msingi na sekondari nchini India kati ya mwaka 1976 na
1987. Kabla ya kuingia rasmi katika siasa mwaka 2000, aliteuliwa kuwa mjumbe
katika Baraza la Wawakilishi na alijihusisha katika biashara ya hoteli.
Mwanasiasa
huyo ni mtoto wa Mkuu wa Kwanza wa Jeshi la Zanzibar baada ya Mapinduzi,
Brigedia Jenerali Yussuf Himid.
Amekuwa akisimamia maridhiano ya Wazanzibari
na Umoja wa Kitaifa akiwa mmoja wa wajumbe sita wa Kamati ya Maridhiano
aliyoshiriki kikamilifu kuyaanzisha mwaka 2009.
Pia ni miongoni mwa
Wazanzibari walio mstari wa mbele kutetea muundo wa Muungano, utakaoipa
Zanzibar mamlaka kamili ya dola.
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Mwenyekiti
Hassan Nassor Moyo (CCM), Eddie Riyami (CCM), Abubakar Khamis Bakari (CUF),
Ismail Jussa Ladhu (CUF) na Salim Bimani (CUF).
Source: Kimwanga B. ( August 2013). CCM yameguka Zanzibar. Retrieved from Mtanzania
No comments:
Post a Comment