Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, August 25, 2013

NEWS ALERT: Mwenyekiti, Mbowe (CHADEMA), wabunge Lissu, Msigwa, Sugu, Silinde washikiliwa polisi


Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, wabunge Tundu Lissu, Peter Msigwa, Joseph Mbilinyi (Sugu), David Silinde na viongozi wengine wa mkoa na Wilaya ya Iringa mjini, akiwemo Diwani Nyalusi, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa, eti kwa kosa la kuzidisha muda wa mkutano.

Polisi wanasema mkutano ulimalizika saa 12.30 badala ya saa 12.00

Swali kwa msingi kwa Polisi, sheria gani wanayotumia katika suala hili. Au ni ule mwendelezo wa kutumiwa na kutumiwa na kutumiwa na kutumiwa.

Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Jeshi la Polisi, zote hazizungumzii muda specific wa kufunga mkutano, bali sun set. Kwa sababu sun set inategemea geographical location. Maeneo kama Kigoma saa 1 jioni, jua linawaka kama vile saa 12.

Ni Sheria ya Uchaguzi pekee, ndiyo inazungumzia muda maalum ambao ni 12.30. Na ni kwa sababu ya mazingira ya equality kwa ajili ya wagombea wote kufanya kampeni ndani ya muda mmoja.

Tutaendelea kuwajuza...

No comments: