Taasisi ya Urejesho wa Maadili ya
Taifa (Taumata) iliyosajiriwa kwa usajiri namna S.A 18827, imesisistiza kuwa
kurejea katika maadili mema ndio ufumbuzi wa matatizo yanayolikabili Taifa kwa
sasa nasio vinginevyo. Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es salaam mkurugenzi wa Taasisi ya urejesho wa maadili ya Taifa
ndugu Joseph Goliama alisema kutoka katika maadili mabaya na kuingia katika
maadili mema ndio ufumbuzi wa matatizo ya Taifa kwa sasa. Alisema kuwa makundi mbalimbali ya
wananchi kuacha maadili mema ya Taifa ndio kumekuwa msingi chanzo na
kiini cha Taifa kupoteza Sauti moja ya kuisikiliza na mwelekeo mmoja wa
kuufuata hali inayosababisha makundi mbalimbali ya wananchi kutokuwa na amani
kutopendana na kutokuaminiana.
Goliama alisema kuwa maadili mabaya
ambayo yanafanya Taifa kupoteza amani, umoja na mawasiliano ni pamoja na
makundi mbalimbali ya wananchi kuwaziana mabaya, kutazamiana mabaya, kuneneana
maneno mabaya, kutendeana mabaya, kuonana kwa jicho baya,kuhusiana kwa uhusiano
mbaya, kufanyiana maamuzi yasiyo ya haki na kusimamiana kwa misimamo isiyo ya
haki. Tunawashauri watanzania wa makundi
yote kurudi katika maadili mema na kuacha maadili mabaya ambayo yanatishia
ustawi na maendeleo ya Taifa letu alisema Goliama. Alitoa mfano na kusema maadili mabaya
ndio yametumbukiza mataifa mengi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe hivyo
akawataka wananchi wa makundi yote kulinda na kutetea maadili mema ambayo
yameifanya Tanzania kuitwa kisiwa cha amani.
Aliitaka serikali kuangalia uwezekano
wakuyakutanisha makundi yote ya wananchi nakuyakalisha pamoja ili yakubaliane
ni Taifa gani yanataka kulijenga litakalohakikishia kila kundi ustawi na
maendeleo endelevu . Akifafanua zaidi alisema wadau wa
amani na umoja wa Taifa ni wananchi wa makundi yote yakiwemo makundi ya dini,
vyama vya siasa, jinsia, rika, wafanyabiashara, wafugaji, wakulima, wafanya
kazi ,Askari nakuyataka makundi hayo kupigania amani na umoja na haki ili Taifa
liapate ustawi na maendeleo endelevu. Goliama
alimalizia kwa kuitaka serikali iishirikishe taasisi ya urejesho wa maadili ya
Taifa katika majukum yake ya kutafuta amani ,umoja na mshikamano wa kitaifa
No comments:
Post a Comment