Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, August 6, 2013

Kiongozi wa CCM matatani kwa tuhuma za ubakaji


       MJUMBE wa Kamati ya Siasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kyela, Joseph Mwaipopo (65) mkazi wa Kijiji cha Fubu, Kata ya Ikama amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kyela akituhumiwa kumbaka na kumsababishia maumivu mtoto wa dada yake (jina linahifadhiwa). Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi wa wilaya hiyo, Nicholaus Tiba, aliiambia mahakama hiyo kuwa tukio hilo lilitokea Julai 16, mwaka huu saa 4:00 asubuhi ambapo mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto wa dada yake wakati wakimwagilia shamba la matikiti. Alidai kuwa mlalamikaji baada ya kufanyiwa kitendo hicho alitoa taarifa ofisi ya serikali ya kijiji na Kituo Kidogo cha Polisi Ipinda ambapo walimpeleka katika kituo cha afya cha Ipinda kwa uchunguzi zaidi.

Mwendesha mashitaka huyo alimweleza Hakimu wa mahakama hiyo, Joseph Luambano, kuwa mtuhumiwa alifikishwa mbele ya mahakama hiyo chini ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 16 ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Mtuhumiwa amekana shitaka na yupo nje kwa dhamana ya sh milioni nne na wadhamini wawili, ambapo kila mmoja dhamana yake inagharimu sh milioni mbili na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 4, mwaka huu.

Source: Yassin I. ( August 2013).Kiongozi wa CCM matatani kwa tuhuma za ubakaji. Kyela. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: