Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, August 24, 2013

Kikao cha CC kutikisa ajenda ya muundo wa serikali tatu


      Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeanza jana jioni huku suala la muundo wa serikali tatu na Viti Maalum, vikitarajiwa kutikisa kikao hicho. 
Mbali na masuala ya Rasimu ya Katiba Mpya, sakata la madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba Mjini, waliofukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera, ni miongoni mwa mambo ambayo pia yanatarajia kukitikisa kikao hicho cha siku moja. Madiwani hao wanane kuwa ni  Yusuph Ngaiza wa Kata ya Kashai ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Bukoba; Samuel Ruhangisa (Kitendagulo); Murungi Kichwabuta (Viti maalumu); Deusdedith Mutakyawa (Nyanga); Richard Gaspal (Miembeni); Alexander Ngalinda (Buhembe) ambaye pia alikuwa Makamu Meya; Dauda Kalumuna (Ijuganyondo) na Robert Katunzi wa Kata Hamugembe.

     Hata hivyo, Halmashauri ya mkoa huo iliamua Ngaiza ataendelea na wadhifa wake wa uenyekiti wa CCM kwa kuwa chama ngazi ya Taifa ndicho kinachoweza kulishughulikia suala hilo. Msimamo wa CCM mfumo wa serikali mbili  kuendelea kuwepo katika Katiba ijayo huku Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ikipendekeza muundo wa serikali tatu. Aidha, baadhi ya wajumbe wa CC walisikika wakitetea uwepo wa Viti Maalum kwa madai kuwa unawasaidia wanawake wengi kupata nafasi za uwakilishi. Kikao hicho kitafuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ambacho kitafanyika kwa siku mbili huku agenda kuu ikiwa ni kuangalia maoni ya wanachama wao juu ya msimamo wa CCM kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya.


Source: Ippmedia (August 2013). Kikao cha CC kutikisa ajenda ya muundo wa serikali tatu. Retrieved from Ippmedia/Nipashe 

No comments: