Leo Chadema Arusha walikuwa na mkutano mkubwa wa shukurani kwa
wakazi wa Arusha kwa kuifanya Chadema iibuke mshindi kwa kunyakua Kata zote nne
zilizoshindaniwa katika uchaguzi uliofanyika mwezi jana ukiambatana na matukio
ya mauaji ya watu wanne kwa shambulio la bomu. Miongoni mwa wahutubiajai ambao
walikuwa kivutio sana kwa maelfu ya watu waliojitokeza katika viwanja vya Shule
ya msingi Ngarenaro kuhudhuria mkutano huo ni Kamanda Alphonce Mawazo...
Akiongea huku anashangiliwa sana, alisema hivi "Kuna damu
ya watoto wadogo, miaka 14 na chini ya hapo. Kuna damu ya wanawake, wababa,
wakristu, waislamu, vikongwe na watu wa rika zote. Wapo waliokufa wapo majeruhi
lakini yote kwa yote hii ni damu ya watanzania wachache iliyomwagika kwa niaba
ya wengi. Hakuna damu chafu na safi linapokuja kwenye swala la ukombozi.
Wanaosema Chadema ni ya kabila fulani au dini fulani wameaibika.
Tumekufa wote kwasababu tunagandamizwa wote na CCM. Kadiri
tunavyopigwa ndivyo tunavyopendana, kushikamana na hata kufiana..."
Kamanda Mawazo akihutubia jioni ya leo Jijini Arusha |
Kina Lema wakiwasili viwanjani hapo na kupokelewa kwa shangwe.. Ulinzi uliimarishwa sana, haikuwa rahisi kuwakaribia viongozi |
Madiwani wapya walipoitwa kusalimia umma |
Source: KanjaPlanter (August 2013). "Kama Hakuna Damu Isiyofaa Kwa Ukombozi, Basi Sisi ni Wamoja" - Mawazo, Mkutano wa CDM Arusha leo. Retrieved from Jamii Forums
No comments:
Post a Comment