Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, August 22, 2013

Dk. Slaa kunguruma Gongo la Mboto kesho


  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho wanatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara Gongo la Mboto, Dar es Salaam kesho Jumamosi. Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake Dar es Salaam jana, Katibu wa CHADEMA Jimbo la Ukonga, Jumaa Mwipopo, alisema mkutano huo utakaofanyika katika viwanja vya Kampala utaanza saa tisa alasiri, na kuwataka wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao kuhudhuria kwa wingi, wakiwamo viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali. Mwipopo alisema lengo la ujio wa kiongozi huyo wa kitaifa wa chama hicho ni kuhutubia mkutano huo kuhusu mabaraza ya Katiba.

     Viongozi wengine wanaotarajiwa kufuatana na Dk. Slaa ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwanasheria wa chama hicho, Mabere Marando na wengine wengi. Vilevile Mwipopo alisema katika mkutano huo uongozi wa CHADEMA Jimbo la Ukonga utagawa rasimu za Katiba bure kwa wananchi wote watakaohudhuria na vijitabu vinavyohusu mapendekezo ya Katiba mpya ya CHADEMA. Akizungumzia kuhusu mkutano mkuu wa jimbo uliofanyika Agosti 18, 2013 ambao ulihusu mapendekezo ya CHADEMA kuhusu Katiba waitakayo Watanzania, alisema ulikuwa wenye mafanikio, kwa sababu watu mbalimbali bila kujali itikadi za vyama vyao maoni yao yalisikilizwa na kuzingatiwa.

     Mwipopo alisema katika mkutano huo aliwahimiza Watanzania kuchangia maoni yao kwa kina kuhusu Katiba mpya, akibainisha kuwa umaskini tulionao umetokana na ubovu wa Katiba. Alishutumu sera mbovu zilizopo za ‘kuwabeba’ wageni (wawekezaji), kwa serikali kuwamilikisha ardhi na kuwaacha wananchi wanyonge wakiteseka bila kuwa na sauti kuhusu ardhi yao inayochukuliwa. “Mwekezaji anapokuja kutoka nje na anataka kuwekeza katika ardhi, aje moja kwa moja kwa mwananchi mwenye ardhi hiyo na aingie naye mkataba mwananchi mwenyewe. Huu ndio moja ya mipango ya CHADEMA ili kumpa mwananchi uwezo wa kumiliki rasilimali ya nchi yake. Lakini tutafanya hivyo kwa kufuta kipengele cha kusema ardhi ni mali ya serikali,” alisisitiza Mwipopo.

Source: Kanyara J. (August 2013). Dk. Slaa kunguruma Gongo la Mboto kesho. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: