Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, August 23, 2013

Dk. Slaa awataka Watanzania kutokubali kuburuzwa Katiba mpya

         Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amewataka Watanzania kutokubali kuburuzwa wala kupotoshwa  na watu wanaotaka madaraka kwa kuweka vifungu vyenye maslahi  yao katika Katiba mpya. Aliyasema hayo mjini hapa wakati chama hicho kilipokuwa kikikusanya maoni ya Rasimu ya Katiba Mpya kwa wanachama wake. “Tusikubali kuburuzwa, tusikubali kudanganywa na chombo chochote hata kama ni Chadema hata kama ni CCM, tunatengeneza Katiba ya Watanzania siyo ya CCM wala siyo ya Chadema,” alisema. 

      Alisema vyama vyote vitaondoka lakini bado Watanzania watabakia katika maeneo yao na kuwataka kuwa makini na watu wanaoshinikiza kuingiza maslahi yao katika Katiba hiyo. Alisema kuwaburuza na kuwapotosha Watanzania katika suala la uundwaji wa Katiba Mpya hakutaleta amani nchini. “Simameni imara, kila mmoja afikirie kwanini tunatengeneza Katiba, ni kwa ajili ya sisi wenyewe, watoto wetu, wajukuu wetu na hata miaka 100 ijayo, wawe na nchi ambayo wataifurahia, watakaa kwa upendo, amani,” alisema na kuongeza; “Lakini si kwasababu vyama tunataka madaraka, kama mtaona Chadema kimeweka kifungu fulani ili kipate madaraka ikatae Chadema kama ni CCM wakataeni pia .”

     Alisema chama cha  CCM kinakataa kifungu katika Rasimu ya Katiba Mpya kinachoondoa wabunge wa viti maalum, kwa kuhofia kupoteza madaraka ya wanawake wengi.  “Wanakataa kwasababu itapunguza wabunge wanawake kutoka 105 na kubakia 30, wale wote zaidi 70 watakwenda wapi kwa hiyo hawa wote wanalinda maslahi yao,” alisema.

Source: Ippmedia (August 2013).Dk. Slaa awataka Watanzania kutokubali kuburuzwa Katiba mpya. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: