Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, August 9, 2013

CHADEMA yavuna wanachama wapya mbeya vijijini



 Katika Kuendelezo kampeni zake za kijiji kwa kijiji, ofisi ya CHADEMA mbeya vijijini leo imefanya mkutano wake katika kijiji cha IPINDA kata ya IHANGO ambapo chama kimefanikiwa kujivunia wanachama wapya zaidi ya hamsini. 
kijiji hicho ambacho kilikuwa ni ngome ya CCM na kupelekea kutoa matokeo mabovu katika uchaguzi mkuu uliopita kimebadilika kutokana na wanachi kutolidhishwa na viogozi wa ccm kuanzia ngazi ya kitongoji mpaka uraisi, katika malalamiko yao mbele ya uogozi wa wilaya wa chama cha demokrasia na maendeleo mbeya vijijini wananchi hao wamemtupia lawama na kutoa madhaifu kibao ya mbunge wa jimbo la mbeya vijijini MCHUNGAJI MWANJALE, wanachi wamedai ahadi zote alizo ziahidi haja timiza zaidi ya kuwapa mpira mmoja vijana kwa ajili ya michezo na shilingi elfu hamsini kuwapa wakina mama kama kifuta jasho kwa ajili ya kazi nzito ya kutengeneza barabara ambalo ni jukumu la halmashauri na vitu alivo toa sio mahitaji ya wanakiji hao kwani wao wanataka shule, barabara. hospitali, maji ambavyo yeye aliahidi.

      Mwana kijiji mmoja mwanamke ( kwenye picha akiongea) amedai hawata kuja kuludia makosa waliyo yafanya kuwapa dhamana viongozi wa CCM kwani mpaka sasa mchango wa shule kila mwana kijiji ametoa sh 40,000 bado 10,0000, shule ya msingi ipo kilomita 20 toka kijijini hapo, maji hakuna na wanatumia kisima kilichopo katika bonde la SIMWAMBALATU ambapo hata mifugo inategemea maji hayo, mchango wa sh 2000 kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa walimu wanao fundisha shule jilani na kijiji, kitendo cha kuhamishwa kata bila majadiliano na wanakijiji hao na kitendo cha mbunge wao kuongea mambo yasiyo yamsingi bungeni na kuacha kuhoji juu ya matatizo makubwa yanayo wakabiri wanachi wa jimbo hili ni moja kati ya sababu chache zilizo wafanya waachane na CCM. wanachama hao wameapa kuto ludia katika siasa za CCM ambazo hazina matumaini kwa maisha yao yajayo. Wakinamama, vijana kwa wazee wameungana na mabadiliko ya kweli kijijini IPIDA.


Source: One Two (August 2013).CHADEMA yavuna wanachama wapya mbeya vijijini .Retrieved from Jamii Forums

No comments: