Nape alisema kuvunjwa kwa Muungano kutasababisha
mgogoro mkubwa wa rasimu kutokana na muda ambao Muungano huo umedumu. Alisema kuundwa kwa serikali tatu si sera ya CCM
kama wanavyodai wapinzani, bali ni maoni ya watu waliyoyawasilisha katika
ukusanywaji wa maoni ya Rasimu ya Katiba mpya. “Sera ya CCM ni kuongoza serikali mbili na si tatu,
na hii sera tutaendelea kuitetea na kuilinda mpaka mwisho wa dunia,
tunachoamini katika chama chetu hatuogopi kutetea sera ambazo tumezitoa
wenyewe,” alisema Nnauye. Alisema ni vyema zikamalizwa kasoro zilipo katika
mfumo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na si kuongeza madaraka yasiyo na
tija. Nape alisema kitendo cha Tume ya Jaji Joseph
Warioba kusema imetumia sheria ya mwaka 1964 kuwa kigezo cha kuundwa kwa
serikali tatu si sahihi, kutokana na makubaliano ya mwaka huo kwamba ni
serikali mbili.
Kiongozi huyo wa CCM pia alishangazwa na kitendo
cha Rasimu ya Katiba mpya kutamka wazi idadi ya mikoa pamoja na wilaya ambazo
zitatumika katika uchaguzi na kwamba mwenye jukumu hilo ni Rais Jakaya Kikwete
na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein. “Serikali ya Muungano chini ya mfumo wa serikali
tatu itaelea katika madaraka, kwani serikali ya Tanganyika itakuwa haiwezi
kuwatetea wananchi, hali itakayosababisha kuwepo kwa mgogoro mkubwa wa urasimu
ambao ni adui wa maendeleo,” alisema Nnauye. Aidha alisema kuwa kuvunjika kwa Muungano
kutasababisha kuiburuza Serikali ya Zanzibar kiuchumi, kwani asilimia 95 ya
uchumi wa visiwani unategemea Tanzania Bara.
Alisema kuwa sera nzuri ya kuwa kiongozi ni
kuwatetea wananchi na si kuwazidishia mizigo. Akizungumzia suala la mgombea binafsi, Nnauye
alisema CCM hakiogopi mgombea binafsi, kwani hata akigombea chama hakitapata
hasara yoyote. Nape alisema sera ya CCM ni kukataa wagombea
binafsi wanaouza unga na si kukataa mgombea binafsi kama ambavyo vyama vingine
vya siasa vinavyodai katika vyombo vya habari. Alisema katika Rasimu hiyo sura ya 9 inazungumzia
umri wa Mbunge kuwa kuanzia miaka 25, lakini kwa CCM suala hilo si sahihi,
kwani wabunge wenye miaka 21 wanawajibika vizuri kuliko wazee.
Source: Khamis
H. ( July 2013). Nape: Waliopendekeza serikali tatu ni wazee wanaosubiri
kufa. Retrieved from Mtanzania
No comments:
Post a Comment