Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimenasa mpango
mchafu wa naibu katibu mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba wa kuwahonga madiwani wa
CHADEMA jimbo la Igunga ili wajiunge na CCM
Madiwani hao 3 akiwemo diwani mmoja wa kata na wawili wa viti
maalumu walimkatalia kata kata .
Diwani wa kata ni yule ambaye baba yake alifanyiwa hujuma ya
kugombea akiwa CCM na kisha mtoto wake akagombea kupitia CHADEMA na wananchi
wakampitisha kwa kishindo
Kwa taarifa za awali ni kwamba CHADEMA baada ya kujulishwa
mipango hii kiliwapongeza madiwani wake kwa kuheshimu dhamana waliyopewa na
wananchi na kuheshimu misingi ya demokrasia.
Aliwaahidi fedha na pia kumuhakikishia diwani huyo wa kata kuwa
endapo angegombea kupitia CCM basi chama chake kingempitisha kwa gharama yoyote
hivyo asiwe na shaka
Ni jambo la ajabu kuwa Mwigulu anafanya siasa chafu za kurubuni
madiwani wahamie chama chake bila kujali maadili ya kisiasa na misingi mipana
ya kidemokrasia huku mamilioni ya kodi za watanzania maskini zikiteketezwa
katika chaguzi pasipo sababu
Taarifa zaidi kuhusu hili zitatolewa pamoja na majina ya
madiwani hao kupitia mamlaka husika kichama.
Kamanda Ben Saanane
No comments:
Post a Comment