Madiwani
wanane wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kati ya madiwani 28 wa
Halmashauri ya Manispaa ya Songea, wamesusia mkutano wa hadhara wa Waziri Mkuu
wa Mizengo, Mizengo Pinda,uliofanyika kwenye viwanja vya manispaa hiyo kwa
madai ya kusimikwa bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano huo. Tukio
hilo lilitokea Jumamosi kati ya saa 8:30 mchana na 9:00 alasiri wakati
madiwani wa halmashauri hiyo wakijiandaa kwenda kwenye mkutano huo wakiwa
tayari wamevaa majoha.
Hata
hivyo, madiwani wanane wa Chadema, waliamua kuvua majoho hayo na kuondoka
kwenye eneo la Manispaa huku wakidai kuwa katika eneo la mkutano kuna bendera
ya CCM kinyume cha utaratibu. Kwa
msingi huo, madiwani wanane wa Chadema walikataa kuudhuria mkutano huo.
Source: Mwakanosya G.Bendera ya CCM
yazua tafrani mkutano wa Pinda. Retrieved from Ippmedia/Nipashe
No comments:
Post a Comment