BARAZA
la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), linatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Bodi
ya Umoja wa Vyama vya Demokrasia Duniani (IYDU), utakaofanyika kuanzia Julai 25
hadi 30, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi, alisema mkutano
huo utafunguliwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na utafungwa na
Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe.
Alisema IYDU inayoundwa na mataifa 81,
katika historia Tanzania inakuwa nchi ya kwanza kuwa mwenyeji wa mkutano huo
kwa nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara.
No comments:
Post a Comment