Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, July 30, 2013

Baadhi ya Watanzania waishio nje ya nchi ni wazito linapokuja suala la Mageuzi ya Tanzania


    Nikiwa miongoni mwa Watanzania waumini wa mageuzi, nimekuwa nikistaajabu kuwaona "baadhi" ya Watanzania wenzetu waishio nje ya Tanzania wakisita sana kuyapokea mageuzi tunayoyahitaji kwa udi na umvumba Watanzania sisi hasa hiki kizazi cha tatu! Huu ni mtazamo wangu, na ninaweza kutofautia na wengi katika hili, lakini kutofautia kwa hoja katika jambo lolote linalokusanya malenga wa wili ni turufu muhimu kwao. Yapo mambo mengi ambayo mimi nimeyaona ni sehemu ya sababu za Watanzania hawa kuwa nyuma katika matakwa ya kimageuzi,

   Kwanza kabisa Watanzania tukubali kuwa silika nikikwazo kikubwa cha mwanadamu kubadilika, na wenzetu hawa bado silika imewaandama vya kutosha!

     Pili Watanzania hawa wanaathiriwa na ubora mimi, hii ni tabia iliyojijenga kwa kizazi cha kiafrika na hususani Tanzania watu kudharauliana, mtu akifika Ulaya basi yeye sasa anajua kila kitu na hawezi jifunza chochote kwa mie Mnyalukolo aliyeniacha Nyololo,

    Hivyo hata hizi harakati za mageuzi tunazoziendesha hapa Tanzania kuna Watanzania wengingine huko Ughaibuni wanatuona ni wapuuzi tu liliokosa darasa na mwangaza,

    Tatu, Watanzania wengi asili ya uwepo wao nje ya nchi upo mikononi mwa serikali na chama tawala, hivyo mahubiri ya mageuzi yoyote kwao ni kelele tu,

     Tano, Balozi zetu huko duniani zinaendesha shughuli zao kwa asili ileile ya mfumo wa chama kimoja, hili linahitaji mageuzi makubwa ili balozi zetu zikubali kukabiliana na fikra mpya za vijana wetu huko waliko!

Hayo ni machache ambayo mimi nimeyaona nisababu za msingi,

Yericko Nyerere/JF

No comments: