Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, June 11, 2013

Wajumbe waridhia Rasimu ya Katiba ya TPSF


       MKUTANO Mkuu maalumu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) umeridhia mabadiliko ya rasimu mpya ya katiba ya taasisi hiyo yatakayosababisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu Julai 25 mwaka huu. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, mkutano huo ni mwendelezo wa mkutano uliofanyika Januari 29, mwaka huu, ikiwa ni mchakato wa kuimarisha sauti moja yenye nguvu ndani ya taasisi hiyo. “Mkutano wa leo unawasilisha mapendekezo ya mabadiliko ndani ya katiba ya TPSF yatakayosababisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu kwa mtindo wa kongamano,” alisema Simbeye kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

         Aliongeza kuwa mtindo wa kongamano ambao ulikubalika, una lengo la kuangalia sekta za uchumi ambapo kila kongamano itapendekeza mtu mmoja ambaye ataweza kuingia katika bodi ya TPSF. “Wajumbe wamekubaliana kwamba mfumo huu mpya utaleta bodi yenye nguvu kwa kuzingatia sekta za uchumi kama zilivyoainishwa katika mikutano ya awali. “…Hivi sasa tunategemea tutakuwa na watu kutoka makundi ya kiuchumi, utamaduni ambao awali tulikuwa hatuangalii uwakilishi wa watu kutoka katika sekta za kiuchumi,” aliongeza. Kwa mujibu wa mapendekezo, wawakilishi wa makongamano kumi ndio wataunda bodi ya TPSF, nafasi moja ikiwekwa kwa mwenyekiti anayemaliza muda wake. Pia makundi maalumu kama wanawake, vijana na walemavu watapewa upendeleo maalumu katika muundo mpya wa TPSF.

Source: Tanzania Daima (Jube 2013).Wajumbe waridhia Rasimu ya Katiba ya TPSF. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: