Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, June 1, 2013

Tumbaku kusababisha vifo milioni nane nchini mwaka 2030

Kushoto ni mapafu mazima, kulia yaliyo athiliwa na tumbaku


       Tafiti zinaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2030, vifo vitokanavyo na bidhaa aina ya tumbaku vitaongezeka hadi kufikia milioni nane ya Watanzania. Pia imebaini kiwango cha wanafunzi wanaotumia tumbaku kwa sasa nchini  ni zaidi ya  asilimia 10.6  kutokana na viashiria vya matangazo mbalimbali ya bidhaa hiyo. Akisoma risala  katika Maadhimisho ya Siku ya Kutotumia Tumbaku  Duniani, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Tumbaku Tanzania (TTCF)), Lutgard Kagaruki, alisema walitegemea  serikali  ingesitisha Mkataba wa Kimataifa wa matangazo yanayochochea bidhaa hiyo tangu  mwaka 2010.

    “Tanzania iliridhia Mkataba wa Kimataifa wa kudhibiti matumizi ya tumbaku mwaka 2007 , hivyo kutokana na matakwa ya mkataba huo ilibidi ipige marufuku matangazo, promosheni, na ufadhili wa tumbaku mwaka 2010” alisema Kagaruki. Alisema TTCF, kupitia wanaharakati wake kimesikitishwa na uamuzi wa serikali wa kutumika kama chambo  cha kuzalisha na kuboresha zao hilo, kwa kisingizio cha kupanua wigo wa soko katika nchi ya China.

        Aliongeza kuwa sambamba na hilo, wanaitaka serikali kupiga marufuku tumbaku aina ya ‘Shisha’, ambayo inatumika katika kumbi mbalimbali za starehe ili kunusuru kundi la vijana ambao wanaitumia bila kujua uhalisia wake. Shisha’, imeingia nchini hivi karibuni,  na imewekwa aina ya viungo kama ‘Vanilla’, ‘Ice Crème’, ‘strawberry’, ambavyo huondoa harufu mbaya ya tumbaku”  

       “Kwa kulitambua hilo, wadau wa afya wakishirikiana na wanaharakati , mashirika ya kudhibiti bidhaa hiyo ndani na na nje, tumeweka mkakati wa kupunguza janga hilo kwa sababu’Dunia bila tumbaku inawezekana , ikisaidiwa na Tanzania bila tumbaku” alisema . Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana, alizitaka taasisi, mashirika pamoja na wadau wa kudhibiti bidhaa hiyo, kuelekeza nguvu kazi huko ili kuokoa wimbi la vijana ambao ni tegemezi sasa na baadaye. “Nitafikisha suala hili kwenye sekta husika ili kuishawishi serikali kuingilia kati hasa kwa kusitisha matangazo, promosheni pamoja na viashiria vyote vinavyoshawishi ongezeko la bidhaa hii”lisema Rugimbana.


Source: Ippmedia (May 2013).Tumbaku kusababisha vifo milioni nane nchini mwaka 2030. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: