Hatimaye
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Kamanda Wilfred Muganyizi Lwakatare
'Lwaks' leo atapata dhamana na kurudi uraiani, baada ya Mahakama ya Kisutu
kuamua kuwa dhamana yake iko wazi na sasa masharti tu ndiyo
yanakamilishwa. Lwakatare anapata dhamana, huku jaribio la watawala kwa
kutumia vyombo vya dola, kutaka kukichafua kwa kukipaka matope ya ugaidi na
mauaji CHADEMA likiwa limeshindwa vibaya.
It's has
been a battle, very seriuos battle, legally and politically, of almost three
months. Bungeni, kwenye majukwaa ya siasa na mahakamani. Fighting for justice,
hopes and dignity of being.
And the
battle still goes on. Aluta continua.
Mapambano
yataendelea kwa sababu sasa tunaanza kuamini kuwa akina Hitler, Botha na
wengine wa namna hiyo bado wanaishi kwa namna nyingine, kupitia baadhi ya watu
waliokabidhiwa madaraka ya kuongoza lakini wameamua kutawala.
Usikubali
kufumbia macho uonevu wowote, mahali popote, kwa mtu yeyote. Ukikaa kimya leo,
akina Hitler wetu hawa wa zamu zetu, watakapokufikia wakati wa 'zamu' yako
hakutakuwa na mtu wa kukusemea.
Ni muhimu
makamanda wasimame kwenye haki, utu, upendo, kweli na matumaini kwa ajili ya
Watanzania hawa wanyonge. Mengine yote yatafuata.
Asanteni
kwa kuonesha nguvu ya umma (people's power) kwa kufuatilia suala hili tangu
siku ya kwanza na hadi litakapofika mwisho kwa namna nyingine linavyoendelea
sasa mahakamani.
Tunaanza
Mungu, tunaendelea Mungu, tutamaliza na Mungu...
Lwakatare ameachiwa kwa
dhamana ya Million 10
Makene
No comments:
Post a Comment