SHIRIKA lisilo la kiserikali la Strengthening the Protected Area Network in Southern Tanzania (SPANEST) limeandaa mdahalo na wadau wa ulinzi na maliasili juu ya wimbi la ujangili wa tembo kwa Nyanda za Juu Kusini. Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake juzi, Mratibu wa mradi wa shirika hilo, Godwel ole Meing’taki, alisema mdahalo huo utajadili kwa undani juu ya tatizo la kukithiri kwa ujangili wa tembo na uharibifu wa mazingira. Meing’taki alisema mdahalo huo utawashirikisha viongozi wa ngazi za juu wa serikali katika ngazi ya mikoa, wilaya, taasisi na mashirika ya serikali, mashirika ya kimataifa na wadau wengine kutoka mikoa iliyoalikwa.
Alisema mdahalo huo wa siku mbili utakaoanza leo katika ukumbi wa Chuo cha Veta mkoani Iringa, utafunguliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii. Balozi Khamisi Kagasheki. “Nina amini michango ya wadau itakuwa mizuri katika kukabiliana na wimbi hili ambalo linatishia kutokomeza kizazi cha tembo katika maeneo ya hifadhi,” alisema Meing’taki.
Source: Mlowe D. (June 2013).Mdahalo ujangili wa tembo kuanza leo. Iringa. Retrieved from Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment