Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, June 9, 2013

Chadema nao wamshupalia Makamba kuhusu uchochezi


    Sakata la kikundi cha ushirika wa wakulima wa chai wa Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga limeingia sura mpya baada ya watu mbalimbali kuunga mkono Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba afikishwe mahakamani kwa kuchochea uasi. Wametaka serikali kumvua unaibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknorojia kwa kuwa kitendo hicho ni cha udhalirishaji wa serikali, jamii ya Watanzania na nchi kwa ujumla. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza kusikitishwa na tukio hilo na kuitaka serikali itoe tamko haraka iwezekanavyo ili kurejesha hali ya amani badala ya hatari iliyotangazwa na baadhi ya watu wakiongozwa na mbunge wa jimbo hilo.

        Ofisa wa chama hicho mkoa, Jonathan Bahweje, alisema kuwa kutokana na matokeo ya vurugu hizo zilizodaiwa kuchochewa na kiongozi huyo, Chadema inaunga mkono bodi ya UTEGA kutaka kumfikisha mahakamani mbunge huyo pamoja na kuitaka serikali ichukue hatua kali ikiwa ni pamoja na kumuondoa kwenye orodha yake ya manaibu waziri ili kulinda heshima ya nchi. Bahweje ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu ametoa siku saba kwa serikali kuhakikisha uasi huo unazimwa na shughuli kiwandani hapo kuendelea ili kumpunguzia hasara zisizo na ulazima mwekezaji huyo na siku 14 nyingine za kumchukulia hatua Makamba.

        Alisema yeye kwa niaba ya chama Mkoa wa Tanga wanalaani vitendo vya kufungiwa nje kwa kufuli walinzi wa kiwanda hicho waliopo wawapo ndani ya kiwanda watu wanaojiita wawakilishi wa wakulima na kwamba hatua hiyo ni ukatiri na ni hatari na ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu.


   Alieleza kuwa kwa kuwa matukio yote ya kihalifu yanayofanywa na wakulima hao yanaelezwa kuwa ni utekelezaji wa maazimio ya mkutano baina yao na mbunge huyo ni wazi kuwa serikali imehusika na vurugu hizo na ili kujisafisha ni kumuwajibisha Makamba aliyeuitisha. “Huyu bwana kwanza ni mvunjaji mkubwa wa demokrasia…ameshawahi kumhujumu aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya Kwekitui kwa tiketi ya Chadema ambaye alitoroka siku mbili tu baada ya Mbunge huyo kufanya ziara kijijini hapo…hii ni hujuma, hafai mtu huyu,” alisema Bahweje.

       Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima wa chai walisema kuwa hakuna ubishi juu ya uvurugu zinzoendelea baina ya muwekezaji wa kiwanda cha chai Mponde na wakulima zimebuniwa na Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba. Baadhi ya wananchi ambao ni wakulima wa zao la chai Jimbo la Bumbuli, walidai kuwa chimbuko la mgogoro huo ni kutokana na masuala ya kisiasa na kwamba hauna tija yoyote. 

      Wakulima hao ambao ni wapigakura wa Makamba ambao walionekana kumgeuka, walieleza kuwa vurugu hizo zinawaathiri kwa kiwango kikubwa na kwamba wanalazimika kula mlo mmoja kwa siku baada ya kiwanda kuzuiwa kufanyakazi. Walidai kuwa sababu ya vurugu hizo ni kutokana na mbunge huyo kutaka kuhakikisha kuwa sehemu zote muhimu anaweka wapambe wake ili kujiweka vizuri kwenye uchaguzi mkuu ujao.  


Source: Masoli M (June 2013).Chadema nao wamshupalia Makamba kuhusu uchochezi. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: