Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, June 2, 2013

CCM: Tuna hoja 12 za kupinga ubunge wa Lissu


        
             CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kina hoja 12 za rufaa ya kupinga ushindi wa ubunge wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema). Akizungumza mjini hapa jana, Mwanasheria wa Chama hicho ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, Glorious Luoga, alisema mambo hayo ni ya kiutendaji na yalifanywa na yeye bila katibu mkuu kushirikishwa, kwa kuwa hayakuhitaji ushiriki wake. “Hapo katikati mahakama ilichelewa kutoa nakala ya hukumu na mwenendo wa mashitaka, ambapo tulipokea 8/3/2013 ndani ya siku 90 toka hapo tukawasilisha Memorandum of Appeal 7/5/2013,” alisema Luoga.

          Alisema sababu za kukata rufaa ni kutokana na hukumu iliyotolewa kuwa na makosa mengi ya kisheria hivyo kuamua kukata rufaa Mahakama ya Rufani. Alizitaja hoja hizo ambazo CCM inazo kuwa ni Jaji kufuta baadhi ya vifungu vya maombi ya kutengua uchaguzi na kuruhusu maombi kuendelea kusikilizwa wakati vifungu hivyo vimefutwa. “Hoja nyingine ni jaji alikuwa akiwazuia mashahidi kueleza baadhi ya ushahidi wao na pia alikuwa akifuta katika kumbukumbu baadhi ya maelezo ya mashahidi,” alisema Luoga.

            Alitaja hoja nyingine kuwa ni pamoja na kaji kukataa kuitwa msimamizi wa uchaguzi kama shahidi muhimu wa kuhojiwa. Alisema hoja nyingine ni jaji kukataa kutumia ushahidi wote uliotolewa na mashahidi ambao ni wanachama wa CCM akidai ni wapambe. Alisema katika hoja nyingine ambayo wanayo ni jaji kukataa kukubali ushahidi uliotolewa na wanachama wa Chadema dhidi ya Lissu na akawaita Turn Court. Alisema jaji alikataa kupokea ushahidi wa CD akidai ushahidi huo Tanzania haukubaliki katika kesi za jinai tu.

         Alisema pia alikubali viapo vya mawakala ambavyo viliapwa kinyume cha sheria na sababu nyingine tano za msingi zinaeleweka. Hata hivyo, alimtaka Lissu kujipanga na kesi iliyopo mbele yake na aache kuingiza siasa na unafiki usio na msingi kwa kuwa asije kulia baadaye. Akizungumzia kuhusu tuhuma za CCM kulipa gharama za kesi hiyo, alisema kesi zote zilizofunguliwa chama hicho kuhusu kupinga matokeo ya uchaguzi, zimegharamiwa na CCM kwa kuwa ni wajibu wake hata kama zimefunguliwa na wanachama. Alitolea mfano kuwa hata Chadema iligharamia kesi ya Deus Mallya aliyekuwa dereva wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe, ambapo wakili aliyemtetea ni Godfrey Wasonga.

Source: Mangala P. (June 2013). CCM: Tuna hoja 12 za kupinga ubunge wa Lissu. Dodoma. Retrieved from Mtanzania

No comments: