YASHINDWA KUWANASUA WENGI
MATOKEO ya kidato cha nne ambayo serikali iliagiza yapitiwe upya na kufanyiwa uhakiki kwa vigezo vya miaka ya nyuma, yametolewa jana huku kukiwa na mabadiliko kidogo. Matokeo hayo mapya yalionyesha hali bado ni mbaya kwani ni watahiniwa 30,000 tu kati ya 240,909 waliopata daraja sifuri ndiyo walionufaika na ‘mbeleko’ ya serikali. Mabadiliko hayo yanaonyesha waliopata daraja sifuri wamepungua kidogo na sasa wamefikia 210,846. Matokeo yanaonyesha kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 9 ambapo mara ya kwanza ilikuwa asilimia 34.5 wakati hivi sasa ni asilimia 43.08. Matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa takriban asilimia 61 ya watahiniwa walipata daraja sifuri awali sasa yamepungua na kuwa asilimia 56.9.
Akitangaza matokeo hayo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema hali bado ni mbaya. Kawambwa alisema kuwa jumla ya watahiniwa 480,029 walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana wakiwemo wasichana 217,587 sawa na asilimia 45 .33 na wavulana 262,442 sawa na asilimia 54.67. Alisema watahiniwa waliofanya mtihani ni 458,139 sawa na asilimia 95.44 ambapo watahiniwa 21,890 sawa na asilimia 4.56 ya watahiniwa wote waliosajiliwa hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali. Alibainisha kuwa matokeo ya watahiniwa wa shule 159,609 kati ya watahiniwa 397,138 waliofanya mitihani walifaulu ambapo wasichana walikuwa 60,751 na wavulana walikuwa ni 98,858.
Kawambwa alisema ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonyesha jumla ya watahiniwa 35,349 wamefaulu katika daraja la 1-111 ambapo kati yao wasichana ni 10,924 na wavulana ni 24,425 sawa na asilimia 43.08. Matokeo ya awali yaliyotangazwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1. Idadi ya watahiniwa waliotangazwa hapo awali na waliotangazwa sasa imeonyesha pia kuwa na tofauti ambapo awali waziri alisema kuwa jumla ya watahiniwa 35,349 wamefaulu katika madaraja 1-111 ambapo kati yao wasichana ni 10,924 na wavulana ni 24,425.
Aliongeza kuwa katika matokeo hayo watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa 68,804 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia 50.30 na wavulana 34,199 sawa na asilimia 49.70 ambapo alisema watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,918 na wavulana 30,083 wamefanya mitihani wakati watahinmiwa 7,803 sawa na asilimia 11.34 hawakufanya mitihani. Alzitaja shule za sekondari zilizoshika nafasi ya kumi katika kundi la shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ni shule ya wasichana St. Fransic iliyoko Mbeya, Marian Pwani (Wavulana) na Feza Boys Dar es Salaam. Shule nyingine ni Canosa, Feza Girls, Rosmini Girls, Anwarite Girls, St. Marys Mazinde Juu na Jude Moshono.
Pia alisema matokeo ya kupangiwa shule watakazotakiwa waende yatafanyika mwezi Juni na wanafunzi wataanza kidato cha sita mwezi Julai. “Tumefanya hivyo, hatukuchakachua na matokeo haya ni halali kabisa hivyo ndiyo yatakayokuwa rasmi kutumika sehemu yoyote na si yale ya awali kama ilivyokuwa mwanzo,” alisema Waziri Kawambwa.
Shule watakazopangiwa
Kawamba alisema watahiniwa hao watapangiwa shule watakazotakiwa waende kuanzia kesho na wanafunzi wataanza kidato cha sita mwezi ujao. “Tumefanya hivyo hatukuchakachua na matokeo haya ni halali kabisa hivyo ndiyo yatakayokuwa rasmi kutumika sehemu yoyote na si yale ya awali,” alisema Kawambwa. Alisema pia baada ya kufanya kwa marekebisho hayo ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 34.5 awali na sasa 43.08 huku akieleza kuwa mwaka 2001 matokeo yalikuwa juu kwa asilimia 53. Hata hivyo alisema kuanzia sasa utatumika mfumo mpya ambapo alama zote zitakuwa sawasawa na hakutakuwa na tofauti za alama katika masomo.
Source: Ban A. (May 2013). MATOKEO MAPYA: Kidato cha nne majanga tena. Retrieved from Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment