MRATIBU wa kampeni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje, ametoa ahadi ya kujenga zahanati ya kata ya Tingeni katika jimbo la Muheza. Bahweje alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Tingeni, Omary Kanyau, uliofanyika kijiji cha Ukoka. Alisema wananchi wa kata hiyo wanauhitaji mkubwa wa huduma za afya kwani zilizopo ziko mbali na kwamba chama hicho kina mipango endelevu na wananchi hao.
Akizungamza kwa niaba ya wakazi wanaoishi katika kata hiyo, Shaban Salim, alisema kwa muda mrefu wanateseka bila kupata huduma za afya, hivyo kuwalazimu kwenda kutibiwa katika hospitali teule ilioko wilayani Muheza. Salim alisema katika kata hiyo mbali na huduma za afya kuna tatizo la daraja ambapo likijaa maji huwezi kuvuka kwenda upande wa pili kitendo kinachopelekea watoto wanaosoma shule katika maeneo hayo kushidwa kuhudhuria masomo kutokana na daraja hilo kujaa maji.
Source: Kilindi E. (May 2013). CHADEMA yaahidi kujenga zahanati Tingeni. Muheza. Retrieved from Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment