Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, March 18, 2013

Wilfred Lwakatare, Ludovick wafikishwa mahakamani


HATIMAYE Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Dk Eliezer Feleshi amemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na mwenzake kwa makosa ya ugaidi.

Mbali na Lwakatare mshitakiwa mwingine ni Ludovick Rwezaula Joseph ambao wanatetewa na mawakili wa kujitetemea Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu na Nyaronyo Kicheere.

Washitakiwa hao wakifikishwa saa mbili asubuhi mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa askari kanzu waliokuwa wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Ilala, Duwani Nyanda na kuhifadhiwa nyuma ya jengo la mahakama hiyo tayari kwa ajili ya kufikishwa kizimbani kosomewa mashitaka yanayowakabili.

Washitakiwa hao waliingizwa ndani ya ukumbi namba moja wa mahakama hiyo saa 7:06 mchana chini ya ulinzi mkali wa wanausalama, huku Lwakatare akiwasalimu wafuasi wa CHADEMA kwa kuwaonyesha ishara ya vidole viwili ambapo wafuasi hao walikuokuwa wamefurika mahakamani hapo tangu asubuhi, wakimjibu kwa kumuonyeshea ishara ya 
vidole viwili juu.

Baada ya kupanda kizimbani, jopo la mawaikili wakuu wa Seriakali linaloongozwa na Mwanasheria Kiongozi wa Serikali Kanda ya Dar es Salaam, Ponsian Lukosi, Purdence Rweyongeza na Peter Mahugo walidai hati ya mashitaka ina jumla ya makosa manne.

  1. Wakili Rweyongeza alililaja kosa la kwanza ambalo linawakabili washitakiwa wote kuwa ni la kula njama kutenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha 284  cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002. Kwamba mnamo Desemba 28 mwaka jana, huko Kimara King’ong’o  Stopover, washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kutaka kutumia  sumu kwa lengo la kumdhuru  Denis Msaki  ambaye ni Mwanahabari wa Gazeti la Mwananchi, kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha 227 cha sheria.
  2. Wakili Rweyongeza alilitaja kosa la pili kwa washitakiwa wote kuwa, kinyume na kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, washitakiwa walitenda kosa la ugaidi la  kula njama kutaka kumteka Msaki  kinyume na kifungu  cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.
  3. Aidha alilitaja kosa la tatu  kuwa ni kutenda kufanya mkutano wa kupanga kufanya makosa ya ugaidi  kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana, walishiriki katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki  kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi.
  4. Wakili Rweyongeza alilitaja shitaka la nne ambalo linamkabili Lwakatare peke yake ni kuwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi, kwamba Desemba 28 mwaka jana, Lwakatare akiwa ni mmiliki nyumba hiyo ilipo Kimaraka King’ong’o  kwa makusudi  aliliruhusu  kufanyika kwa kikao hicho baina yake na Ludovick  cha kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka nyara Msaki.

Washitakiwa wote walikanusha mashitaka hayo.

Wakili Rweyongeza  alidai kuwa makosa  hayo yameletwa chini ya sheria mbili tofauti yaani kosa la kwanza linaangukia katika sheria ya Kanuni ya Adhabu lakini kosa makosa yaliyosalia yanaangukia kwenye Sheria ya Kuzuia Ugaidi na kwa kuwa makosa yanaoangukia kwenye sheria ya ugaidi huwa  hayana dhamana, ni Mahakama Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Wakili Rweyongeza aliieleza mahakama kuwa Jamhuri inawasilisha ombi la pili ambapo wanaiomba mahakama imruhusu mshitakiwa wa pili (Ludovick) aende kukaa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kwa sababu Jeshi la polisi linamuiitaji kwa ajili ya hatua za kiupelelezi zaidi.

Hata hivyo, mawakili wa utetezi Peter Kibatala aliomba mahakama iwapatie wateja wake dhamana na kwamba suala la washitakiwa kupatiwa dhamana au kunyimwa ni la mahakama.

Kwa upande wake, wakili Lissu alidai aliita hati ya mashitaka kuwa ni kipande cha karatasi kilichowasilishwa na DPP-Dk Feleshi ambacho akionyeshi nembo ya serikali, mhuri na wala hiyo hati ambayo aliipachika jina la kipande cha karatasi kuwa hakikuletwa mahakamani hapo kwa ridhaa ya DPP na kuiomba mahakama hiyo isiiamini hicho kipande cha karatasi kuwa ni nyaraka halali ya Serikali.

Kwa upande wake wakili Profesa Abdallah Safari aliomba mahakama irejee kesi za kubambikizwa zilizowai kufunguliwa mahakamani hapo na ofisi ya DPP miaka ya nyuma ikiwemo kesi ya mauji ya fundi majeneza wa Manzese ya mwaka 2002, iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Sheikh Issa Ponda na Sheikh Kundecha ambapo yeye alikuwa akiwatetea washitakiwa hao ambapo alilazimika kwenye kuonana na DPP wa wakati huo ambaye ni Jaji Mstaafu kwa sasa, Juxon Mlai na kumueleza kuwa kesi ile ya mauji ni ya kubambikwa ambapo Mlai alitumia mamlaka yake kuifuta.

“Katika kesi hii ya Lwakatare ninachokiona ni matumizi mabaya ya sheria na wale waliombakizia kesi Lwakatare wanastarehe na kufurahi kuona Lwakatare anaenda kuishi gerezani,”alidai Profesa Safari.

Akipangua hoja za mawakili hao wa utetezi, wakili wa serikali Rweyongeza alidai kuwa hoja hizo tatu zilizowasilishwa na mawakili wa utetezi ni dhaifu na: “tunaomba mahakama itambue kuwa kesi hii imefunguliwa na upande wa Jamhuri na wala haijafunguliwa na chama cha siasa.”
 
Kuhusu hoja ya kuwabambikizia kesi washitakiwa hao, Rweyongeza ambaye alikuwa akionyesha kujiamini alidai kesi hiyo siyo ya kubambikiziwa na kwamba ofisi ya DPP inafanyakazi yake kwa mujibu wa sheria  na haipo kwa ajili ya kubambikia watu kesi. Akadai ikiwa Profesa Safari ana ushahidi wa Lwakatare kubambikiwa kesi, basi aende kuonana na DPP na ampatie huo ushahidi unaonyesha washitakiwa wamebambikiwa kesi.

Akiijibu hoja ya Lissu kuwa DPP amewasilisha kipande cha karatasi kisicho na kibali cha DPP, wakili Rweyongeza alimtaka Lissu aache kasumba ya kuongea mambo bila ya kufanya utafiti kwani DPP amefungua kesi hiyo na amewasilisha kibali chake mahakamani hapo (wakili huyo alilitoa kibali hicho kama kielelezo hali iliyofanya watu kuanza kuangua vicheko).

Aidha, kuhusu hoja ya kutaka washitakiwa wapatiwe dhamana, wakili Rweyongeza alidai kuwa sheria ya ugaidi imetungwa na bunge ambapo kifungu cha 49 cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi kinakataza kabisa mshitakiwa anayeshitakiwa kwa makosa yanayoangukia kwenye sheria ya ugaidi kupewa dhamana, hivyo kwa kuwa washitakiwa hao makosa yanayowakabili yanaangukia kwenye ya ugaidi, mahakama haiwezi kuwapa dhamana.

“Sasa nawashangaa hawa mawakili wa washitakiwa leo hii wanajifanya hawajui matakwa ya kifungu cha 49 cha sheria ya ugaidi kinasema nini. Sheria ya ugaidi imetungwa na Bunge hivyo ni sheria halali. Kama mawakili wa utetezi wanaona sheria hiyo ni mbaya, basi haraka sana nawashauri waende Mahakama Kuu wafungue Kesi ya Kikatiba ya kupinga kifungu hicho cha sheria ya ugaidi,  lakini kwa sasa sisi tunasema sheria ya ugaidi ipo kihalali na ndiyo imetumika kuwashitaki washitakiwa hawa,”alidai wakili Rweyongeza.

Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru alisema amesikiliza hoja za pande zote na atatoa uamuzi Machi 20, 2013 na kuamuru washitakiwa wote wapelekwe gerezani, huku akiikataa hoja ya wakili Kibatala iliyotaka Lwakatare apewe dhamana.

Source: Katabazi H. (March 18, 2013). Wilfred Lwakatare, Ludovick wafikishwa mahakamani. Dar es salaam. Retrieved from Wavuti

No comments: