Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, March 29, 2013

Wabunge wamng`ang`ania Waziri Maghembe


Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, jana ilikataa kupitisha bajeti ya Wizara ya Maji kwa maelezo kuwa haikidhi mahitaji ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya miradi ya maji nchini. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Prof. Peter Msola, aliyasema hayo jana wakati wa kupitisha makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14. Alisema kutokana na mapungufu hayo kamati imeagiza wizara kuiboresha bajeti hiyo ili iweze kukidhi matakwa ya miradi ya maji nchini kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo muhimu.

“Tumewaelekeza warekebishe bajeti hiyo kwa sababu kuna maeneo ambayo wameyasahau na tunajua mahitaji ya maji kwa wananchi wengi bado ni makubwa hasa maeneo ya vijijini,. tunataka bajeti hiyo ijibu kero za msingi za wananchi, tutakutana nao tena wiki ijayo,” alisema Prof. Msolla. Aidha, Kamati hiyo iliiagiza Wizara kurudi serikalini na kuomba fedha zaidi kwakuwa fedha iliyopangiwa haiwezi kukidhi utekelezaji wa miradi ya maji nchini. Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maji mwaka wa fedha 2013/2014 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji ni kiasi cha Sh. 379,443,220,000 ambapo Sh. 138,266,164,000 ni fedha za ndani na Sh. 241,177,056,000 ni fedha za nje. 

Source: James R. (March 2013). Wabunge wamng`ang`ania Waziri Maghembe. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: