WAZIRI MKUU PINDA AINGILIE KATI; WIZARA NA TANESCO HAWAJAJIBU UKWELI KUHUSU MGAWO WA DHARURA WA UMEME
Wizara ya Nishati na
Madini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kwa nyakati mbalimbali kati ya
tarehe 28 Februari na 2 Machi 2013 kupitia baadhi ya vyombo vya habari wametoa
majibu yasiyokuwa ya kweli juu ya mgawo wa dharura wa umeme uliotokea mwezi wa
Februari.
Katibu Mkuu wa Wizara
Eliackim Maswi na Afisa Habari wa TANESCO Badra Masoud wote wameeleza kwamba
hakukuwa na mgawo wa umeme bali kilichotokea ni matatizo madogo madogo ya
mitambo na kwamba matengenezo yanaendelea.
Kwa nafasi yangu ya
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ninazo taarifa kwamba ukweli ni kuwa
umetokea mgawo wa umeme wa dharura kutokana na upungufu zaidi wa kina cha maji
katika mabwawa ya kufua umeme, upungufu wa fedha za kununua mafuta mazito ya
kuendesha mitambo ya kufua umeme wa dharura na upungufu wa gesi asili ya
kuendeshea mitambo ya kufua ya umeme.
Hivyo, Waziri Mkuu
Mizengo Pinda anapaswa kuingilia kati kuwaeleza ukweli wananchi ikiwemo hatua
zilizochukuliwa kuhakikisha kwamba hali hiyo haiendelei mwezi Machi kinyume na
ahadi iliyotolewa bungeni tarehe 28 Julai 2012 kwamba mgawo wa umeme ungekuwa
historia.
John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa
Nishati na Madini
02 Machi 2013
No comments:
Post a Comment