Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, March 24, 2013

Makala: Ni hofu ama ubabe kwa CHADEMA?


SERIKALI imezuia maandamano yote yaliyokuwa yafanywe na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Machi 25 mwaka huu katika mikoa ya Mbeya na Arusha. Katika zuio hilo ambalo kwa mara ya kwanza limetolewa kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene badala ya Jeshi la Polisi kama utaratibu ulivyo, serikali inasema hatua hiyo ni kutokana na ukweli kwamba tarehe hiyo Watanzania watakuwa wanampokea Rais mpya wa China, Xi Jinping. Katika sababu hizo, serikali inadai kuwa licha ya CHADEMA kutaka kuandamana siku hiyo kushinikiza serikali kuwawajibisha Waziri wa Elimu na Naibu wake wajiuzulu kufuatia matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012, hata Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitaka kuandamana kupinga kufanyika kwa maandamano hayo.

Serikali inasema kuwa CCM ilitaka kuandamana wakieleza kwamba wana imani na tume maalum ya Waziri Mkuu inayochunguza tatizo la kufeli vibaya kwa wanafunzi hao. Mwambene kwa niaba ya serikali anaongeza kuwa tume hiyo inaendelea na uchunguzi wa suala la kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne 2012, hivyo si vyema vyama vya siasa vya CCM na CHADEMA vikaingilia mchakato huo wa uchunguzi. Sisi tunaona zuio hili ni woga na ubabe wa serikali kwa CHADEMA kutokana na sababu dhaifu zilizotolewa, tena kupitia idara ambayo kiutaratibu siyo inayohusika kutoa taarifa za kuruhusu ama kuzuia mikusanyiko. CHADEMA walitangaza muda mrefu kufanya maandamano yao hayo, hatukuwahi kusikia sababu za CCM nao kutaka kuandamana hata ratiba ya ujio wa Rais wa China vili vile nayo ilikuwa ya kificho.


Kwa serikali kuyazuia maandamano ya wananchi kudai elimu bora kwa ajili ya watoto wao kwa kisingizio eti inawapa nafasi ya kumpokea Rais wa China ni kituko ambacho hata Wachina wakisikia watatudharau milele. Tunachelea kuanini kuwa hatuwezi kufanya mambo yetu eti kwa sababu tu yanaingiliana na ratibu ya ujio wa wageni. Huku ni kutojitambua matatizo yanayotukabili kama taifa. Hoja ya serikali kama isingekuwa ni ubabe na hofu kwa CHADEMA, isingeweza kutumia idara yake ya maelezo kutangaza zuio hilo bila kukutana na waratibu wa maandamano hayo na kujadiliana ili wapangiwe tarehe nyingine kwenye mikoa ambayo ugeni huo wa China ungefika.

Kwa mujibu wa seria za vyama vya siasa, mikutano na maandamano huratibiwa na Jeshi la Polisi na hivyo chama husika hutakiwa kuwasilisha taarifa ya maandishi kwa jeshi hilo ndani ya saa 48 ili kupatiwa ulinzi. Sasa hili la CHADEMA inakuwaje taarifa ipelekwe polisi halafu wajibiwe na Maelezo? Tunadhani iko haja ya serikali yetu kujitathmini na kujaribu kujiepusha na aibu wakati mwingine kwani hata ingetokea leo Rais Jakaya Kikwete anafanya ziara nchini China, Wachina wasingezuiwa kufanya mambo yao ya msingi kwa sababu hiyo.

Source: Tahariri (March 2013). Ni hofu au ubabe kwa CHADEMA. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: