MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewafutia kesi ya makosa ya
ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph baada ya
Mkurugenzi wa Mashitaka( DPP), Dk Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya kuwafutia
kesi hiyo washitakiwa kwa sababu hana haja ya kuendelea nayo.
Sambamba
na hilo, DPP ilimfungulia kesi ya makosa ya ugaidi upya Lwakatare na
Ludovick ambapo kesi hiyo mpya namba Na.6/2013 ambapo imepangiwa kwa
hakimu mpya Aloyce Katemana.
Katika kesi ya ugaidi Na.37/2013 iliyofunguliwa
na Jamhuri dhidi ya Lwakatare na wenzake Machi 18 mwaka huu, ambayo ilifutwa
saa tatu asubuhi na ambayo ilikuwa imekuja kwa ajili ya Hakimu Mkazi, Emilius
Mchauru kuitolea uamuzi wa ama wa kuwapatia dhamana washitakiwa au la, hakimu
Mchauru alijikuta akishindwa kutoa uamuzi wake kwa sababu mawakili
viongozi wa serikali Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na Peter Mahugo
waliwasilisha hati hiyo ya DPP chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya
Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, ambapo kifungu hicho kina mpa
mamlaka DPP, kuifuta kesi yoyote ya jinai muda wowote kabla ya haijatolewa
hukumu na uamuzi huo wa DPP haujahojiwa
Source: Jackson A. (March 2013). Lwakatare atupwa Rumande hadi Apri 3, baada ya kufunguliwa mashtaka mapya. Retrieved from Audiface Jackson blog
No comments:
Post a Comment